Alikiba akanusha kuandaa watu wamzomee Diamond kwenye Fiesta
Alikiba amekanusha uvumi unaodai kuwa huenda aliaandaa watu maalum wa kumzomea Diamond Platnumz kwenye show ya Fiesta iliyofanyika ...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/10/alikiba-akanusha-kuandaa-watu-wamzomee.html
Alikiba amekanusha uvumi unaodai kuwa
huenda aliaandaa watu maalum wa kumzomea Diamond Platnumz kwenye show ya
Fiesta iliyofanyika October 18 katika viwanja vya Leaders Club jijini
Dar es Salaam.
“Hamna ukweli wowote, naanzaje?,”
amehoji. “Siwezi kufanya kitu kama hicho. Kikubwa ni kuwashukuru wana
Dar es Salaam walivyonipokea, nimefurahi sana. Hii imenitia moyo na
kunifanya niongeze bidii kuwaandalia vitu vizuri zaidi.”
Katika hatua nyingine, msanii huyo
amesema mashabiki wa muziki wake wasishangae kuona video ya wimbo wa
‘Mwana’ wiki hii ama wiki ijayo. “Video ni muda wowote yaani, usishangae
ukasikia video imetoka. Muda wowote video inatoka surprise, kwahiyo
waendelee kusubiri muda wowote.”
