BAADA YA UCHUMBA KUVUNJIKA! ROSE NDAUKA HATAKI TENA MWANAUME Wednesday, October 15, 2014 Kunn Mursal 0 Udaku ...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/10/baada-ya-uchumba-kuvunjika-rose-ndauka.html
BAADA YA UCHUMBA KUVUNJIKA! ROSE NDAUKA HATAKI TENA MWANAUME
SIKU chache baada ya uchumba wake kuvunjika, msanii
wa filamu Bongo, Rose Ndauka amefunguka na kusema kuwa kwa sasa haitaji
tena mwanaume kwani anajikita zaidi katika kufanya kazi.
Akizungumza na gazeti hili juzikati, Rose alisema katika maisha yake
ya uchumba alijifunza mambo mengi na anamshukuru Mungu amempa zawadi ya
mtoto hivyo anafanya kazi kwa bidii ili aweze kumlea mwanaye vizuri.
Alisema hajutii kwa yaliyomtokea kwa mchumba wake Malik Bandawe,
kwani makosa yaliumbwa makusudi ili watu wapate kujifunza, hivyo akili
yake kwa sasa anaiwekeza katika kazi zake za sanaa.
