BAADA YA KUTALAKIANA DIDA AZIKA RASMI NDOTO ZA KUOLEWA
NDOA basi! Mtangazaji wa Kituo cha Redio cha Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida’ amezima ndoto za kuishi maisha ya mke na mume kwa kud...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/10/baada-ya-kutalakiana-dida-azika-rasmi.html
NDOA basi! Mtangazaji
wa Kituo cha Redio cha Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida’ amezima ndoto za
kuishi maisha ya mke na mume kwa kudai kuwa, amebaini kujiingiza kwenye
ulimwengu huo ni kujipa ‘stress’ za kujitakia.
Akizungumza
na Ijumaa Wikienda juzi, Dida alisema baada ya kuachana na aliyekuwa
mume wake, Edzen Jumanne, amebaini wanaume wote lao ni moja hivyo kama
atakubali kuingia kwenye ndoa na mwanaume mwingine, itakuwa ni yaleyale.
“Yani
sasa hivi hata aje mwanaume na gia gani siwezi kukubali kuolewa tena,
kwa kifupi sina ndoto za kuitwa mke wa mtu tena, bora nibaki peke yangu
nifanye mambo yangu,” alisema Dida.
