Alichosema Cheik Tiote kuhusu tuhuma za kuwa na wake wawili na ‘hawara’
http://samchardtz.blogspot.com/2014/10/alichosema-cheik-tiote-kuhusu-tuhuma-za.html
Hivi karibu gazeti la The Sun liliripoti juu ya tuhuma za kumhusu kiungo wa timu ya Newcastle Cheick Tiote na familia yake.
Tiote,
ambaye anavuna kiasi cha paundi £45,000 kwa wiki kupitia klabu yake ya
Newcastle, ameripotiwa kufunga ndoa ya kimila na Laeticia Doukrou mwezi
uliopita, japokuwa tayari ameshaoa mke mwingine aitwaye – Madah mwenye
umri wa miaka 25.

Tiote na mke mpya
Kiungo
huyo mwenye miaka 28, kwa sasa anaishi na Madah pamoja na watoto wao
wawili katika jumba lao lenye thamani ya £1.5million Ponteland karibu na
Newcastle, pia Tiote ana mtoto mwingine nje ya ndoa zake na mwanamke wa
nje aitwaye Nikki Mpofu.
Wakala
wa mchezaji huyo Jean Musampa amethibitisha kuhusu mchezaji kuoa mara
ya pili, alisema: ‘Ninachoweza kusema ni kwamba ni kweli ameoa na hiyo
ni ndoa yake ya pili.
‘Hiki
ni kitu cha kawaida, Tiote ni muislam, sheria za kidini zinamruhusu
kuoa hadi wake wanne, hivyo hakuna kibaya alichofanya.This is nothing
unusual. He is a Muslim.’
Tiote pia anaripotiwa kuwaambai marafiki zake kwamba haoni shida kuwa na wanawake wengi, na hata nyumbani kwao Ivory Coast ameshwakuwa na mahusiano na wanawake wengi. Gazeti la The Sun limeripoti.
Tiote pia anaripotiwa kuwaambai marafiki zake kwamba haoni shida kuwa na wanawake wengi, na hata nyumbani kwao Ivory Coast ameshwakuwa na mahusiano na wanawake wengi. Gazeti la The Sun limeripoti.
Gazeti
hilo pia limeripoti kwamba mahusiano kati ya Tiote na ‘hawara’ yake
Nikki Mpofu yamefikia ukingoni baada ya miaka mitatu baada ya mwanamke
huyo raia wa Zimbabwe kuchoshwa na ahadi za uongo za kuolewa na mchezaji
huyo.

