Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba Watishiwa Maisha
http://samchardtz.blogspot.com/2014/09/wajumbe-wa-bunge-maalumu-la-katiba.html
Siku
tatu kabla ya Bunge la Katiba kuanza kupigia kura Rasimu ya Katiba
inayopendekezwa, watu wasiojulikana wameanza kusambaza vitisho vya
kuwatia hofu wajumbe wa Bunge hilo.
Watu hao wamesambaza vipeperushi katika maeneo mbalimbali ya mji wa
Dodoma usiku wa kuamkia jana, wakiwataka wajumbe kutoingia bungeni
vinginevyo yatakayowapata watajuta, huku wajumbe kutoka Zanzibar
wakitishiwa kwa ujumbe wa simu kupitia mtandao wa WhatsApp.