JINSI YA KUFANYA ILI USIFUNGIWE ACCOUNT YA GOOGLE ADSENSE KWENYE BLOG/WEBSITE YAKO
Google adsense ni bidhaa moja wapo ya Google ambayo huwapa chance wamiliki wa blogs na website kujipatia kipato kutokana na matan...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/09/jinsi-ya-kufanya-ili-usifungiwe-account.html
Google
adsense ni bidhaa moja wapo ya Google ambayo huwapa chance wamiliki wa
blogs na website kujipatia kipato kutokana na matangazo mbali mbali ya
makampuni ambayo google huyapokea na kuwapa bloggers kuyaweka kwenye
blogs/website zao na mwisho wa siku una pata commision kutoka na idadi
ya watu waliotembelea blog/Website yako na walio click matangazo ...
Nimeona
niongelee hii issue kutokana jinsi baadhi ya bloggers wanavyolalamika
kwani kila wakijaribu kujiunga baada ya muda wanafungiwa account kwa
kukiuka masharti ya google adsense...Baadhi ya blogger ambao
niliwasaidia kutengeneza google adsense nao pia kuna walio fungiwa na
kurudi kwangu wakitaka niwatengnezee nyingine huwa naona huruma sana as
ni pesa inahusika tena na unakuta ni blogger mchanga
Kwa kifupi hawa jamaa wana masharti mengi kidogo na ukiyakiuka wanakutumia message kama hii hapa chini :
"Hello,
With our advertising programs, we strive to create an online ecosystem
that benefits publishers, advertisers and users. For this reason, we
sometimes have to take action against accounts that demonstrate behavior
toward users or advertisers that may negatively impact how the
ecosystem is perceived. In your case, we have detected invalid activity
in your AdSense account and it has been disabled"
Hapo ndio unakuwa umefungiwa hata kama ulikuwa na balance ambayo ulikuwa
unategemea utumiwe mwisho wa mwezi ndio basi tena Google wanairudisha
kwa advertisers...
Sasa kuna kuna Masharti mengi lakini
mimi nitaongelea matatu tu ambayo naweza sema ndio wengi hufungiwa
account zao kwa ajili hiyo ....
1. Don't click on your own Google ads (Usibonyeze Matangazo ya google wewe mwenyewe kwenye blog yako)
Hilo ni Tatizo hasa kwa bloggers wachanga huwa wanataka kujaribu kila
kitu wakishakuwa na blog ...So wakishakuwa na google adsense wanajaribu
kuclick yale matangazo waone nini kitatokea ama tu kwa kutaka
kujiongezea hela....Ila jua kwamba google adsense wameweka robots za
ambazo zinaangalia IP adresses , wewe kama Admin ukitumia hiyo Computer
yako kubonyeza matangazo wanajua ni wewe unajitafutia hela so at the end
of the day watakufungia ....Watu wanaohitajiwa kuclick ni visitors
wengine sio wewe mwenye blog...
2.Impressions (Sijui kiswahili chake
vizuri ila hii ni ile wewe as admin kufungua fungua au kuview blog yako
wewe mwenyewe mara kwa mara)
Kwa uzoefu wangu naweza sema hili ndio tatizo kubwa linalofanya Google
adsense account nyingi kufungwa, hili tatizo ukisoma kwenye policy zao
hawajalielezea vizuri lakini limewaumiza wengi sana nikiwemo mimi , mimi
kabla sijajua nimeshawahi kufungiwa account mbili mwaka 2010 lakini
nilipata solution mpaka leo naenjoy Google money.
Napenda kusema kuwa ukishakuwa na google adsense kwenye Blog/Webiste
yako unatakiwa uwe mpole..kazi yako iwe kupost tu, kuview ulichopost
achia visitors....Wengi tuna tabia ukishapost habari unaifungua na wewe
kuangalia imekaaje hii inasend invalid impression to google kwasababu
kila impression au mtu anapoview blog kuna hela inaingia kwenye account
yako ya Google so ukiwa unafungua wewe mwenye mara kwa mara Robots zao
zinaona kama unacheat na kujitafutia hela mwenyewe...So basi angalau
view blog yako mara moja kwa siku ukiangalia mara kwa mara unajiweka
katika hatari ya kufungiwa.....
Kama utashindwa hilo la kuview blog yako basi weka ADBLOCKER kwenye Browser yako unayotumia kuview blog ..Adblocker ni extension katika brower inayozuia matangazo kuonekana..Ukiwa umeinstall Adblocker Kwenye Browser yako Matangazo ya Google yanafichwa so itakusaidia...Mimi nimefanya hivyo ....
3. Adult Content,
Hii
nadhani inaeleweka tu , hii naweza sema hutakiwa kupost mambo ya ngono
ngono sana ...iwe picha ama maneno makali ..(Katika hili tuna advantage
moja kwa lugha ya kiswahili bado hawajaweka maneno mengi ya kiswahili
katika Robots zao Ila wale wakizungu wanaipata fresh....
Mwisho napenda kusema Google Adsense ni njia nzuri sana ya kujipatia
kipata bila longo longo as longer as una visitors wengi kwenye blog
yako
--------------------------
John Kiandika via udakuspecially