TANZANIA TUNAENDEKEZA MAJUNGU, WENZETU INDIA WAPELEKA CHOMBO SAYARI YA MARS!
India imewakilisha 'Mangalyaan katika sayari ya Mars
http://samchardtz.blogspot.com/2014/09/tanzania-tunaendekeza-majungu-wenzetu.html
Wanasayansi wa anga za juu nchini India wanasema kuwa chombo chao cha safari za anga za juu kwa sasa kinazunguka sayari ya Mars.
Hii
ndiyo mara ya kwanza kwa India kutuma mtambo wake kwenda kwa sayari
hiyo, safari ambayo imepata umaarufu kutokana na gharama yake ya chini
kabisa ya dola milioni 75 pekee.
India ndilo taifa la nne duniani kufaulu kufikisha chombo katika sayari ya Mars.
Mataifa
mengine ambayo yamewasilisha vyombo vya utafiti wa anga za juu katika
sayari hiyo ni Marekani Urusi na muungano wa mataifa ya Ulaya.
Chombo hicho ''The Mangalyaan robotic probe'' kinatarajiwa kuanza upekuzi na uchunguzi wa hali ya anga katika sayari hiyo nyekundu.
Waziri
muu nchini India Narendra Modi ambaye alishuduia mafaniko ya chombo
hicho kilichoanza safari yake miezi kumi iliyopita aliwapongeza
wanaayansi hao kwa ufanisi huo mkubwa.
Aliwaambia kuwa mafanikio ya safari za anga za ju nchini India ni mfano mwema wa hatua ambazo taifa hilo linaweza kupiga akisema kuwa ana mpango wa kuboresha kitengo hicho.
Shirikisho
la anga za mbali la Marekani NASA ambalo lilifikisha chombo chake
''Maven'' katika sayari ya Mars Jumatatu wiki hii, liliwapongeza
wanasayansi wa India kwa ufanisi wao.
Kupitia
kwa ujumbe wa mtandao wa Twitter NASA iliandika kuwa ''Tunawapongeza
@ISRO kwa kuwasili katika sayari ya Mars. Mtajiunga na @MarsOrbiter
kutathmini hali ilivyo katika sayari hiyo".
CREDIT: BBC
