TAARIFA YA KLABU YA SIMBA JUU YA KUUMIA MLINDA MLANGO WAKE IVO MAPUNDA
http://samchardtz.blogspot.com/2014/09/taarifa-ya-klabu-ya-simba-juu-ya-kuumia.html
Zikiwa zimebakia wiki mbili kabla ya
kukutana na mahasimu wao wa jadi, Simba imepata pigo kubwa katika timu
kwa sababu kipa namba moja wa timu hiyo Ivo Mapunda amevunjika kidole
mazoezini Zanzibar jana asubuhi na anatakiwa kuwa nje ya uwanja kwa wiki
nane.
Hatoweza kusimama golini wakati tiu yake
ikicheza na Yanga October 12 2014 ambapo daktari wa Simba SC Yassin
Gembe amesema Ivo aliumia wakati anachupia mpira katika mazoezi ya
asubuhi na kwa bahati mbaya mpira ukamgonga kwenye kidole kidogo cha
mwisho mkono wa kulia.
Gembe amesema Ivo alitoka mazoezini baada ya tukio hilo na baadaye akapelekwa hospitali ya Mnazi Mmoja kisiwani humo ambako baada ya vipimo ikagundulika amevunjika sana.
“Si
kuvunjika kwa mzaha, amevunjika sana na anatakiwa kupumzika kwa wiki
nane, baada ya hapo aanze taratibu… ina maana makadirio ya kurudi tena
uwanjani ni hadi baada ya miezi mitatu‘ – Gembe.
Kuumia kwa Ivo kunatoa nafasi kwa makipa
chipukizi Hussein Sharrif ‘Cassilas’ na Peter Manyika kujibidiisha ili
kuziba pengo lake ambapo sasa Ivo anafanya idadi ya wachezaji majeruhi
ambao ni tegemeo Simba kufikia wanne baada ya Paul Kiongera anayetakiwa
kuwa nje wiki sita, Haroun Chanongo na Issa Rashid ‘Baba Ubaya’.