SUAREZ AFUNGA MABAO MAWILI BARCA B IKIUA 5-0 MECHI YA KIRAFIKI
http://samchardtz.blogspot.com/2014/09/suarez-afunga-mabao-mawili-barca-b.html
MSHAMBULIAJI Luis Suarez amefunga mabao mawili akiwa na jezi yaBarcelona
kwa mara ya pili, timu B ikiitandika 5-0 timu ya taifa ya vijana ya
Indonesia chini ya miaka 19.
Nyota huyo wa Uruguay na mchezaji
mwenzake mpya, Thomas Vermaelen –
ambaye pia alifunga walicheza mechi hiyo ya Barca B kujiweka fiti kabla ya kuanza kuchezea kikosi cha kwanza.
Suarez
haruhusiwi kuchezea Barca mechi za mashindano hadi Oktoba 24
atakapomaliza kutumikia adhabu yake ya kumng’ata Giorgio Chiellini
katika Kombe la Dunia.
Suarez anatarajiwa kuanza kuitumikia rasmi Barcelona katika mechi na Real Madrid Oktoba 24 kwenye La Liga.
Winga David Babunski na Bicho nao pia