SAGUDA AKABIDHI MALI ZOTE ZA MAREHEMU RECHO UKWENI..
ALIYEKUWA mchumba wa marehemu Rachel Haule ‘Recho’, George Saguda amesema ameamua kupeleka mali zote za marehemu kwa ndugu zake il i wa...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/09/saguda-akabidhi-mali-zote-za-marehemu.html
ALIYEKUWA
mchumba wa marehemu Rachel Haule ‘Recho’, George Saguda amesema ameamua
kupeleka mali zote za marehemu kwa ndugu zake ili wao wajue utaratibu wa kuzitumia.
George Saguda akiwa na aliekuwa mchumba wake marehemu Rachel Haule
‘Recho’ Akizungumza na paparazi wetu, Saguda alisema kwa sasa hahusiki
na suala la mirathi ya Recho japo alikuwa akiishi na marehemu kama mke wake na kudai kuwa mali zote zilizokuwa zinamhusu Recho, tayari amezikabidhi kwa ndugu zake.
“Marehemu Recho nilikuwa nikiishi naye kama mke wangu lakini mali
zake zote nimeshazikabidhi kwa ndugu zake kwa sababu wao ndiyo
wanaohusika na suala zima la mirathi endapo kutakuwa na ulazima wa
kunishirikisha basi wataniambia,” alisema Saguda.