Pichaz za magari mapya ya Polisi mtaani Dar es salaam.
http://samchardtz.blogspot.com/2014/09/pichaz-za-magari-mapya-ya-polisi-mtaani.html
Kama
uko town Dar es salaam unaweza ukawa umeshakutana na hizi gari mpya za
Polisi kwenye maeneo mbalimbali ambapo hata usiku zimeonekana katika
baadhi ya maeneo ya mji zikifanya doria.Kwa kipindi kirefu tulizoea kuona Defender zikiwa gari pekee za Polisi kufanya doria kwenye maeneo mbalimbali ya nchi lakini sasa zimekuja hizi mpya ambazo vilevile zinavutia na kuifanya Dar es salaam kuwa miongoni mwa majiji yenye magari mazuri ya kufanyia doria.
Naendelea kufatilia kujua kama magari haya ni kwa ajili ya Polisi Dar es salaam au yamesambazwa kwenye miji mbalimbali.


