Picha: H.Baba na mkewe Flora Mvungi wapeana tuzo, sherehe zafana
Msanii wa muziki H.Baba akishirikiana na mke wake Flora Mvungi Jumamosi ndani ya Giraffe Ocean View Hotel wamefunga ukame wa tuzo kwa...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/09/picha-hbaba-na-mkewe-flora-mvungi.html
Msanii
wa muziki H.Baba akishirikiana na mke wake Flora Mvungi Jumamosi ndani
ya Giraffe Ocean View Hotel wamefunga ukame wa tuzo kwa kupeana wenyewe
kwa wenyewe baada ya kuona kila mmoja kati yao ana mchango kwenye muziki
na filamu.
Tuzo
hizo zinazotambulika kama ‘Tuzo za kifamilia’ zilihudhuriwa na rais wa
shirikisho la filamu Tanzania, Simon Mwakifamba, rais wa shirikisho la
muziki, Ado Novemba, wanafamilia mbalimbali pamoja na waandishi wa
habari na zilifanyika kama tuzo zingine zilivyo.
Wengine walioibuka na tuzo ni Muongozaji mkongwe wa filamu Jully Tax pamoja na mtoto wa H.Baba ‘Tanzanite’.
Rais wa shirikisho la filamu Tanzania Simon Mwakifamba akimkabidhi tuzo Flora Mvungi ya muigizaji bora wa kike
Akizungumza
na wadau mbalimbali, H.Baba ambaye amepata tuzo ya mtumbuizaji bora wa
muziki, alisema yeye ndio msanii anayestahili kupata tuzo kama hiyo kwa
Tanzania.
H.Baba akizungumza huku akiwa ameshika tuzo yake
“Tuzo
hii hapa ni ya mtumbuizaji bora Tanzania,” alisema muimbaji huyo. “Mimi
nina tuzo ya East Africa mtumbuizaji bora, Tanzania sina hata tuzo moja
kwa sababu ya nini nimeshatangaza
naanzisha hii tuzo kwa akili timamu na wala sivuti bangi. Mimi sivuti
sigara wala sinywi pombe, kama kuna msanii anaona hii tuzo sio halali
yangu mimi ajitokeze. Promota yoyote ajitokeze huyo msanii alipwe pesa
mimi nita- perform bure na awadhihirishie watanzania kwamba yeye ni
mkali ya stage Tanzania. Kama
ananizidi mimi, promota amlipe yeye ila mimi kama H.Baba nitaperform
bure na nitakuja peke yangu na yeye inatakiwa aje peke yake. Kwa sababu
kuna Kiswahili fasaha ambacho kinakosewa kuna neno linaitwa mtumbuizaji
bora na kuna watumbuizaji bora. Mimi ni mtumbuizaji bora, wengine ni
watumbuizaji bora,” alijinadi H.Baba.