Obama:Tumekadiria vibaya nguvu ya IS
Rais Barack Obama wa Marekani
http://samchardtz.blogspot.com/2014/09/obamatumekadiria-vibaya-nguvu-ya-is.html
Rais Obama amekiri katika televishen ya kitaifa kuwa Mashirika ya Marekani yalikosea katika kukadiria hatari ya wapiganaji wa dola ya kiislam, Islamic State nchini Iraq na Syria.
Hata hivyo Obama amesema wapiganaji hao waliwahi kuvurumishwa huko Iraq na majeshi ya nchi yake yakishirikiana na kabila la Sunni.
Obama amekiri vyombo vya Ujasusi vya Marekani zilikadiria vibaya uwezo wa majeshi ya Iraq kupambana na wapiganaji wa kiislamu ambao wameteka maeneo mengi nchini humo.
