NYOTA WA CHELSEA EDEN HAZARD AIPIGA 'TEKE LA TUMBO 'PSG
+4 Kiungo wa Chelsea , Eden Hazard amesema hataki kuondoka Chelsea
http://samchardtz.blogspot.com/2014/09/nyota-wa-chelsea-eden-hazard-aipiga.html

EDEN Hazard amekanusha taarifa za kuondoka Chelsea kwenda Paris Saint-Germain – licha ya miamba hiyo ya soka ya Ufaransa kuendelea kuvutiwa naye.
Nyota huyo aliyeshinda tuzo ya mchezaji kijana ya PFA msimu uliopita kwa muda mrefu alihusishwa kujiunga na kikosi cha Laurent
Blanc majira ya kiangazi mwaka huu, lakini Jose Mourinho alisema
atasikiliza ofa itayozidi paundi milioni 150 ili kumuachia mchezaji
wake.
Licha ya kuanzia soka lake Ligue 1 kabla
ya kujiunga na Chelsea kwa paundi milioni 32 mwaka 2012, Hazard alisema
hana nia ya kuondoka klabuni hapo kurudi alikotoka.

Kutokana na kiwango chake, The Blues
wanatarajia kumzawadia namba 10 huyo mkataba wa miaka mitano ambapo
atalipwa mshahara wa paundi laki mbili kwa wiki na anatarajia kutia
saini mwezi ujao.
"PSG wapo ulimwengu ule ule kuliko Chelsea," Hazard aliwaambia Canal+ .
"Lakini kama wanataka kuwa klabu ya kiwango cha juu wanatakiwa kushinda
ligi ya mabingwa. Nimeridhika Chelsea, ni sehemu ambayo nilipenda
kuendelea kukua. PSG hawapo kichwani mwangu"