Nick Cannon akanusha kuwa chanzo cha Amber Rose kuomba talaka kwa mumewe
Baada ya taarifa za Amber Rose kudai talaka kwa mumewe Wiz Khalifa, mume wa Mariah Carey, Nick Cannon ambao nao ndoa yao imevunjika,...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/09/nick-cannon-akanusha-kuwa-chanzo-cha.html
Baada
ya taarifa za Amber Rose kudai talaka kwa mumewe Wiz Khalifa, mume wa
Mariah Carey, Nick Cannon ambao nao ndoa yao imevunjika, amekanusha
uvumi kuwa yeye ndio chanzo cha Amber kuomba talaka.
Nick
Cannon ambaye kwasasa ndie meneja mpya wa kazi za Amber Rose, amedai
kuwa hakuna kitu chochote zaidi ya kazi kinachoendelea kati yao.
Vyanzo vimeiambia TMZ kuwa, Nick amekuja kufahamu kuwa Amber ana matatizo ya kifamilia kupitia mwanasheria wake wiki iliyopita baada ya kusaini nae mkataba kama mteja wake, na ndipo alipofahamu kuwa ndoa ya Amber ina matatizo.
Vyanzo mbali mbali vimedai kuwa Amber na Wiz kila mmoja anamshutumu mwenzake kwa kuchepuka.
