Mwasiti afunguka show zinazomlipa zaidi Bongo, Pia Kuachia nyimbo mbili 'Leo f/ Godzilla' na 'Kisigino' hivi karibuni
Mwadada anayetamba na ngoma yake ya Serebuka, Mwasiti ni mmoja kati ya wasanii wa kike ambao hawaonekani sana kwenye shows za uwanja...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/09/mwasiti-afunguka-show-zinazomlipa-zaidi.html
Mwadada anayetamba na ngoma yake ya Serebuka, Mwasiti ni mmoja kati ya
wasanii wa kike ambao hawaonekani sana kwenye shows za uwanjani lakini
mwenyewe anasema kuna shows zake zinazomuingizia pesa nyingi zaidi.
“Nafikiri watu wengi hawanionagi kwenye shows za uwanjani sana
lakini kuna shows zangu ambazo nikipiga mpunga napiga pesa ya maana sana
(anacheka).”
“Kuna vijana wanapenda sana Zouk Rhumba huwezi amini. Na kuna wa umri fulani sasa wale wa miaka 35 kwenda juu wanapenda sana Zouk Rhumba, kwa hiyo wale huwa wana corporate shows, viongozi na nini.
Mwasiti akitoa Burudni katika Moja ya Show za Fiesta
“Kwa hiyo mara nyingi nafanya hizo sana kuliko zile za uwanjani ambazo wengi wanategemea kuniona, za vijana zaidi. Kibiashara iko vizuri as long as unatoa kazi ambayo wataielewa.”
Ameongeza.
Mwasiti anatarajia kuachia nyimbo mbili hivi karibuni. ‘Leo’ aliomshirikisha Godzilla na ‘Kisigino’.
Mwasiti anatarajia kuachia nyimbo mbili hivi karibuni. ‘Leo’ aliomshirikisha Godzilla na ‘Kisigino’.