MTOTO WA NDEGE ZANZIBAR' AANIKA UCHAWI WAKE ,RPC APIGWA BUTWAA
SAKATA la mtoto Happiness (10) aliyetikisa kwa tukio la kupanda ndege kutoka jijini Dar es Salaam kwenda Zanzibar bila kujulikana limei...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/09/mtoto-wa-ndege-zanzibar-aanika-uchawi.html
SAKATA la
mtoto Happiness (10) aliyetikisa kwa tukio la kupanda ndege kutoka
jijini Dar es Salaam kwenda Zanzibar bila kujulikana limeibuka tena, safari hii katika sura mpya kufuatia mtoto huyo kufungua kinywa chake na kuanika mambo ya kichawi, Uwazi lina mkanda mzima.
Mtoto Happiness (10) anayeishangaza jamii kwa matukio ya kimazingara.
Mtoto
huyo aliyaanika mambo hayo mwishoni mwa wiki iliyopita mbele ya Kamanda
wa Mkoa wa Kipolisi Ilala, Dar, SACP Mary Nzuki na kumfanya afande huyo
kupigwa butwaa. Aidha, alizungumza na Uwazi, nyumbani kwao, Mkuranga.
ALICHOSEMA AWALI NI HIKI
Awali
akizungumza kwa kujiamini, mtoto huyo ambaye ni mkazi wa Kijiji cha
Mkokozi Kata ya Vikindu wilayani Mkuranga, Pwani, alikiri kusafiri kwa
ndege hadi Zanzibar akidai alikwenda kumfuata baba yake mzazi aishiye
huko.
Hata
hivyo, mama yake mzazi, Sarah Zefania alimpinga mwanaye huyo na kusema:
“Baba yake haishi Zanzibar, yupo Kipunguni (Ilala jijini Dar es
Salaam).”
Mtoto Happiness akiwa na mama yake
KUHUSU UCHAWI
Mtoto
Happiness alikwenda mbele zaidi kwa kujiongeza akisema katika maisha
yake amekuwa akifanya mambo ya kishirikina lakini si peke yake. Alisema
ana mshirika wake (hakumtaja jina).
Happiness aliutaja
ushirikina huo. Alisema amekuwa akisafiri usiku mara kwa mara na
mshirika wake huyo wa karibu kwa kutumia usafiri wa ungo!!
ATAJA PAKA, NYOKA NA MBUZI
Kama
vile haitoshi, mtoto huyo ambaye ametokea kushangaza wengi huku
akipachikwa majina ya ‘mtoto wa ndege’, ‘mtoto wa uchawi’ na ‘mtoto wa
miujiza’, alisema akiwa katika safari hizo amekuwa akiwaona paka, nyoka
na mbuzi.
AFIKA POPOTE BILA KUJALI UMBALI
Aliongeza kuwa, kwa kutumia ungo na huyo mshirika wake, wamekuwa na uwezo wa kufika popote wanapopataka bila kujali umbali.
Mkoba ukiwa na nguo za Mtoto Happiness
MAVAZI YA SAFARINI
Akizidi
kufunguka, Happiness alisema mara nyingi wanapokuwa katika safari hizo
ambazo alisema watu hawawezi kuwaona, huvaaa nguo nyeupe, nyeusi au
wakati mwingine nguo nyekundu ili kufanikisha masuala yake ya usiri.
Mtoto
huyo aliyasema hayo kufuatia Septemba 16, mwaka huu kudakwa tena maeneo
ya Feri jijini Dar akiwa na begi ambapo alisema anamfuata baba yake
(hakusema wapi).
Baada
ya walinzi wa eneo hilo kumgundua ni ‘mtoto wa ndege’ walimfikisha
Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar ambapo mama yake aliitwa.
Mama
alishtuka baada ya kumwona mwanaye akiwa amebeba begi lililokuwa na
nguo kwa madai ya kuwa alikuwa akielekea kwa baba yake mzazi.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Ilala, Dar, SACP Mary Nzuki
SIKU YA KUTOROKA MARA YA PILI
Akisimulia
kisa cha kutoroka mara hii ya pili, Happines alisema siku ya tukio mtu
mmoja ambaye alidai kuwa ni kaka yake wa kambo alifika nyumbani na
kumchukuwa yeye na begi lake la nguo akidai anampeleka kwa baba yake
Zanzibar lakini baada ya kufika Feri mtu huyo alitokomea kusikojulikana.
KAULI YA MAMA
Wakati
mama huyo (pichani) akizungumza na Uwazi alimtaka baba wa mtoto huyo,
Julius kujitokeza ili kunusuru hatima mbaya ya mtoto wao.
WACHUNGAJI WANENA
Waandishi wetu waliwatafuta baadhi ya wachungaji wa makanisa ya kiroho nchini ili wazungumzie tukio la mtoto huyo.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, Zakary Kakobe.
NI MAPEPO
Mchungaji
wa Kanisa la Paradise International la jijini Dar, Gideon Parapanda
alisema tatizo linalomsumbua mtoto huyo ni pepo mchafu wa kuzimu hivyo
kwa kutumia maombi ndani ya makanisa hali hiyo itatoweka.
“Happiness
kama alizaliwa salama na hali hiyo imemkuta ukubwani na kufanya mambo
ambayo hayaeleweki ni pepo wachafu ambapo akimtumainia Yesu tatizo hilo
litaisha mara moja,” alisema Mchungaji Parapanda.
WAZAZI WASIENDE KWA WAGANGA
Naye
Mchungaji wa Kanisa la Cathedral of Joy, pia ni Nabii John Komanya,
yeye alisema Happiness anasumbuliwa na pepo wachafu, kitu pekee ni
maombi na alitahadharisha wazazi au ndugu wasiende kwa waganga wa
kienyeji.
ASKOFU KAKOBE ATAKA APELEKWE FULL GOSPEL
Askofu
Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, Zakary Kakobe yeye
alisema matatizo ya Happiness yataisha kwa Jina la Yesu kama ndugu,
walezi au wazazi wataamua kumfikisha kanisani kwake.
“Kinachomsumbua mtoto
huyo ni roho chafu, akiombewa katika makanisa ya kiroho atafunguliwa,
hata kama ndugu wakiamua kumleta hapa Full Gospel ni sawa tu,
atakombolewa,” alisema Kakobe.



