MASHEIKH NA MAPADRE KUSAKATA KABUMBU UWANJA WA TAIFA OCTOBA 12 2014.
http://samchardtz.blogspot.com/2014/09/masheikh-na-mapadre-kusakata-kabumbu.html
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi
Mussa Salim (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa
habari Dar es Salaam leo kuhusu maandalizi ya mchezo wa kirafiki wa
mpira wa miguu kati ya Masheikh na Mapadre utakaofanyika uwanja wa Taifa
Octoba 12-2014. Alhadi Salim ndiye ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya
maandalizi wa mchezo huo. Kushoto ni Katibu wa Kamati ya Amani kutoka
Kanisa la Anglikana Padri John Solomon na Mwakilishi Mkazi wa Shirilka
la KAS,Tanzania Stefan Reith.
Mwakilishi Mkazi wa Shirilka la KAS,Tanzania Stefan Reith (kushoto), akimkabidhi baadhi ya vifaa vya michezo Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, SheikhAlhadi Mussa Salim kwa ajili ya maandalizi wa mechi hiyo.
OKTOBA
12 mwaka huu katika kuadhimisha siku ya amani duniani viongozi wa dini
wanatarajia kujitupa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, wakiwa
na lengo la kudumisha amani iliyopo nchini.
Mtanange
huo utawajumisha Masheikh,Maimamu,Maaskofu,Wachungaji na Mapadre na
mgeni rasmi katika mchezo anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
ambaye tayari amekubali kuungana na viongozi hao wa dini.
Akizungumza
jana jijini, Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye ndiye Mwenyekiti wa
Kamati ya maandalizi ya mchezo huo alisema kuwa Mkuu wa Mkoa huo, Said
Sadick atakuwa mwamuzi msaidizi akisaidiwa na Kamishna wa Kanda Maalumu,
Seleman Kova na Afande IGP Ernest Mangu atakuwa mpuliza kipyenga wa
kati.
Alifafanua
kuwa viongozi hao wa dini tayari wameshaanza mazoezi kwa jili ya
kujiweka tayari kwa ajili ya kufanya vizuri katika mtangane huo wa
kuhamasisha amani na ulivu nchini katika uwanja wa Kumbukumbu ya Karume
jijini Dar es Salaam.
Aliongeza kuwa wanaendelea na mazoezi hayo chini ya kocha mjerumani na Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam, itazipeleka timu mbili mkoani Morogoro kwa ajili ya kujifua zaidi na mtanage huo utakaokuwa wa kukata na shoka kutokana na jinsi timu za viongozi hao wa dini zilivyojipanga kucheza mchezo huo wa amani.
Ili
kujindaa vema na mchezo huo Mwakilishi Mkazi wa Shirilka la
KAS,Tanzania, Stefan Reith, jana alikabidhi Sheikh kwa Dar es Salaam,
Alhad Salum vifaa mbalimbali vya michezo ikiwemo mipira, jeszi na viatu.