Mariah Carey adaiwa kuzama kimahaba kwa muongozaji wa filamu
http://samchardtz.blogspot.com/2014/09/mariah-carey-adaiwa-kuzama-kimahaba-kwa.html
Mariah
Carey anadaiwa kuanzisha uhusiano wa kimapenzi na muongozaji wa filamu,
Brett Ratner baada ya ndoa yake na Nick Cannon kuvunjika.
Muimbaji huyo, 44 anadaiwa kuwa karibu na muongozaji huyo, 45, kumsaidia kusahau kuachana na Nick waliyedumu kwa miaka sita.
Carey
na Ratner walianza kuwa marafiki baada ya muongozaji huyo kuongoza
video za nyimbo zake Heartbreaker na We Belong Together. Carey pia
aliungana na Ratner kwenye uzinduzi wa filamu ya Hercules aliyoiongoza na inaaminika kuwa wawili
hao walikuwa pamoja kwenye likizo huko Aspen mwezi December.
Cannon
alithibitisha kuachana na Carey mwezi August baada ya miezi kadhaa ya
mgogoro katika ndoa yao na amesisitiza kuwa anachojali sasa ni wanae
mapacha, Moroccan na Monroe.
