MANUEL PELLEGRINI ANG'ATA MANENO JUU YA MKONGWE FRANK LAMPARD
+6 Frank Lampard alifunga mawili dhidi ya Sheffield katika mechi ya raundi ya tatu ya kombe la Capital One
http://samchardtz.blogspot.com/2014/09/manuel-pellegrini-angata-maneno-juu-ya.html
Frank Lampard alifunga mawili dhidi ya Sheffield katika mechi ya raundi ya tatu ya kombe la Capital One
KOCHA wa Manchester City, Manuel
Pellegrini ameshindwa kukanusha taarifa za kutaka kumbakisha Frank
Lampard katika dimba la Etihad zaidi ya muda uliopo kwenye mkataba wake
wa mkopo kutoka timu dada ya New York City FC.
Lampard anatakiwa kurudi Marekani mwezi
januari, lakini mkongwe huyo aliyesawazisha bao dhidi ya klabu yake ya
zamani ya Chelsea mwishoni mwa wiki iliyopita na kufunga mengine mawili
jana katika ushindi wa 7-0 dhidi ya Sheffield, kombe la Capita one ameonesha thamani kwa City licha ya kuwa na miaka 36.
Jana usiku shabiki mmoja alivamia uwanja wakati mechi inaendelea na kufanikiwa kupiga picha na nyota huyo wa zamani wa England.
Lampard pia alifunga dhidi ya Chelsea mwishoni mwa wiki katika mechi ya ligi kuu England.
Akizungumza baada ya mechi jana,
Pellegrini aliulizwa kuhusu taarifa za kumbakisha Lampard kwa msimu
mzima, lakini hakusema chochote zaidi ya kusema: "Ni jambo ambalo
tutaliangalia baadaye. Tutaona nini kinatokea januari na tuna miezi
miwili au mitatu ya kuamua".
"Anastahili sifa zote anazopata kutoka kwa mashabiki. Tutafanya kila linalowezekana kwa timu na mchezaji".