JASHO LAZIDI KUMTOKA BOSI WA MANCHESTER UNITED LOUIS VAN GAAL
+4 Louis van Gaal anatoa jasho baada ya Chris Smalling (pichani juu) kuumia.
http://samchardtz.blogspot.com/2014/09/jasho-lazidi-kumtoka-bosi-wa-manchester.html
HOFU imezidi kundanda nafasi ya beki wa kati ya Manchester United baada ya Chris Smalling kupata majeruhi jana jumatano.
Imefamika kuwa Smalling aliumia mguu
katika mazoezi ya kujiandaa na mechi ya jumamosi ya ligi kuu England
dhidi ya West Ham katika uwanja wa Old Trafford.
United watampima leo ili kujua ukubwa wa
majeruhi hayo, lakini Louis van Gaal anasubiri kwa hamu kujua kama beki
huyo wa England atakuwa fiti kucheza.
Tayari United watawakosa mabeki wa kati Phil Jones, Tyler Blackett na Jonny Evans (katikati)
Phil Jones alipata maumivu ya nyama za
paja, Jonny Evans alipaya majeruhi katika kipigo cha 5-3 dhidi ya
Leicester City baada ya kuumia kifundo cha mguu, kabla ya Tyler Blackett
kutolewa nje kwa kadi nyekundu.