MANGULA AFUNGUA OFISI MPYA YA CCM-CHATO
http://samchardtz.blogspot.com/2014/09/mangula-afungua-ofisi-mpya-ya-ccm-chato.html
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM)
kwa upande wa Tanzania Bara Mhe. Philip Japhet Mangula katikati akikata
utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Jengo jipya la Ofisi ya CCM wilaya ya
Chato. Wengine katika picha ni Mbunge wa Chato Mhe. Dkt. John Pombe
Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Geita Said Magalula, Mwenyekiti wa CCM
mkoa wa Geita Joseph Msukuma.
Mbunge wa Chato ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi Dkt.
John Pombe Magufuli katikati akiwa pamoja na Makamu Mwenyekiti wa
Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa upande wa Tanzania Bara Mhe. Philip
Japhet Mangula kulia mara baada ya kumpokea katika kata ya Buseresere
Mkoani Geita. Kushoto ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita ndugu
Joseph Msukuma
Mbunge wa Chato ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi Dkt.
John Pombe Magufuli kushoto akiwa pamoja na Makamu Mwenyekiti wa
Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa upande wa Tanzania Bara Mhe. Philip
Japhet Mangula juu ya gari akihutubia mamia ya wakazi wa Buseresere
mara baada ya kuwasili katika eneo hilo.
Wananchi wa Buseresere wakimsiliza Mbunge wa Chato
ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli wakati alipopita
kwenda kumpokea Makamu Mwenyekiti wa CCM kwa upande wa Tanzania
Bara Mhe. Philip Mangula.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM)
kwa upande wa Tanzania Bara Mhe. Philip Japhet Mangula akisalimiana
na baadhi ya wananchama wa CCM katika kata ya Bwanga wilayani Chato
mara baada ya kusimama kwa muda akiwa njiani kuelekea Chato kwa ajili
ya Ufunguzi wa Ofisi Mpya ya CCM wilaya ya Chato.
Taswira ya Jengo jipya la Ofisi ya Chama cha Mapinduzi
CCM wilayani Chato ambalo ilikuwa ni ahadi ya Mbunge wa Chato ambaye
pia ni waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM)
kwa upande wa Tanzania Bara Mhe. Philip Japhet Mangula akihutubia
wananchi wa Bwanga waliofika kumsalimia wakati akiwa njiani kuelekea
Chato ambapo alizindua jingo jipya la Ofisi hiyo ya kisasa.
Kijana wa Kikundi cha Ngoma cha Chato akionyesha
umahiri wake wa kuzungusha ringi la Tairi la baiskeli kwenye mboni yake
ya jicho hali iliyowashangaza wananchi wengi waliofika.
Mbunge wa Chato ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi
Dkt. John Pombe Magufuli kulia akifurahia jambo pamoja na Makamu
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa upande wa Tanzania
Bara Mhe. Philip Japhet Mangula.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM)
kwa upande wa Tanzania Bara Mhe. Philip Japhet Mangula akivuta utepe
kuashiria ufunguzi rasmi wa Ofisi ya CCM wilaya ya Chato ambayo ilikua
ahadi ya Mbunge wa Jimbo hilo.