LAMPARD HUENDA AKAONGEZWA MKATABA MAN CITY BAADA YA KUITUNGUA CHELSEA
http://samchardtz.blogspot.com/2014/09/lampard-huenda-akaongezwa-mkataba-man.html
KIUNGO
Frank Lampard anaweza akarejea Uwanja wa Stamford Bridge mwezi
Januari, mwakani na kikosi cha Manchester City baada ya kugundulika
kwamba muda wake wa kupiga kazi Etihad umeongezwa.
Lampard,
ambaye amekuwa gwiji wa Chelsea baada ya kuitumikia kwa miaka 13,
alikaribia kumwaga machozi baada ya kutokea benchi Jumapili na kuifungia
City bao la kusawazisha katika sare ya 1-1.
Kufuatia kuonyesha kiwango kizuri kwa
ujumla kwenye mchezo huo na hata
mazoezini,
City sasa wanataka kumuongezea mkongwe huyo mwenye umri wa miaka
36 muda wa mkataba wake wa mkopo kutoka New York City FC ya Marekani
waliomsajili
baada ya kutemwa na Chelsea mwishoni mwa msimu uliopita.
Sasa
huenda Lampard akaichezea City dhidi ya Chelsea Januari 31 mwakani,
hiyo ikiwa ni mara ya kwanza kurejea Stamford Bridge tangu aondoke
mwishoni mwa msimu kuelekea New York City FC.