LAANA YA KANUMBA YAIMALIZA BONGO MUVI
IMEVUJA! Kuvunjika kwa Kundi la Bongo Movie Unity kumedaiwa kuwa ni laana ya aliyekuwa memba hai wa kundi hilo, marehemu Steven Kan...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/09/laana-ya-kanumba-yaimaliza-bongo-muvi.html
IMEVUJA!
Kuvunjika kwa Kundi la Bongo Movie Unity kumedaiwa kuwa ni laana ya
aliyekuwa memba hai wa kundi hilo, marehemu Steven Kanumba kutokana na
kumnyanyapaa enzi za uhai wake, Ijumaa linakupa mchapo kamili.
TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo
makini, Kanumba alikuwa ni miongoni mwa waasisi wa kundi hilo lakini
kabla hajafa, yaliibuka majungu ambayo yalimsababisha ajiengue na
kususia kundi hilo huku akiwa na kinyongo moyoni.
Wakilia juu ya kaburi la marehemu Kanumba.
“Kanumba
hakufurahishwa na majungu yaliyokuwa yakiendelea ndani ya klabu dhidi
yake, akajiapiza kwamba hatakaa akashiriki masuala ya kundi hilo hadi
pale wahusika watakapojisafisha.
“Wakati sisi tukipanga
yetu, Mungu naye anapanga yake. Kanumba alifariki wakati ambao wasanii
waliomsukia majungu hayo hawajajisafisha, kama si kumuomba msamaha,”
kilisema chanzo.
Staa wa filamu Bongo, Jackline Wolper.
KATIBU ASAKWA
Baada ya kunyaka maelezo
hayo ya chanzo chetu, mapaparazi wetu walianza kuwatafuta waliokuwa
viongozi wa klabu hiyo na kufanikiwa kumpata aliyekuwa katibu msaidizi,
Devotha Mbaga, ambaye alikiri kwamba klabu hiyo ina laana ya Kanumba.
HUYU HAPA DEVOTHA
Akizungumza kwa hisia
kali maeneo ya nyumbani kwake Kigamboni, jijini Dar, Devotha alisema
mgogoro unaoendelea ndani ya kundi hilo ambalo linapumulia mashine baada
mwenyekiti wao, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ na katibu wake, William
Mtitu kujiuzulu ni laana ya Kanumba hivyo wanatakiwa kuomba radhi
kaburini kwake.
Staa katika tasnia ya filamu Bongo,Wema Sepetu.
Alisema
enzi za uhai wa Kanumba baadhi ya wasanii ambao wanagombana chini kwa
chini kwa sasa ndani ya kundi hilo (majina yapo), walimnyanyapaa na
walikuwa wakimchukia na kufikia hatua ya kuwakataza wanachama wote
kutoshiriki kwenye filamu zake.
“Ukweli
baadhi ya wasanii hasa hao viongozi wanatakiwa kutambua makosa
waliyomfanyia Kanumba enzi za uhai wake na wamuomba msamaha kwani
walimkosea sana na wakishaomba, naamini Bongo Movie itasimama lakini
wasipofanya hivyo hiyo laana itaendelea kuwatesa na watapigana kila
siku.
“Yaani
kuna wakati hadi huwa nafikia hatua ya kusema bora Kanumba alikufa
mapema yawezekana Mungu alikuwa na kusudi lake maana angeaibika na
angeonekana ni mtu asiyefaa katika jamii kutokana na mikakati ambayo
wasanii wenzake walikuwa wameipanga,” alisema Devotha.
Aliyekuwa mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Stive Mengere.
KUMBE WALIWAHI KUKAA KIKAO
Kama hiyo haitoshi,
katika aya nyingine, Devotha alisema kuna wakati waliwahi kuweka kikao
cha kusameheana kilichoandaliwa na Ridhiwan Kikwete ambaye sasa ni
Mbunge wa Chalinze kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) lakini mambo
bado yakawa ‘shagala baghala’.
“Nakumbuka
kwenye kikao kimoja ambacho aliitisha Ridhiwan Kikwete kwa ajili ya
wasanii na kusema kama kuna mtu amemkosea mwenzake wasameheane baada ya
kuongea na sisi na kuondoka, watu walianza kuongea maneno mabaya ya
kashfa na hapo ndipo walipopanga mikakati ya kumchafua na kutofanya kazi
na Kanumba lakini baada ya siku chache alifariki.
Staa katika tasnia ya filamu Bongo, Vincent Kigosi 'Ray'.
“Hao
wanaogombana sasa hivi ndiyo walikuwa vinara katika kumnyanyapaa
Kanumba na ndiyo haohao siku ya mazishi yake ndiyo waliobeba jeneza,
msalaba na kuvaa suti wakati walikuwa hawako naye vizuri, unajua roho
huwa haifi kwa hiyo wanatakiwa kuomba msamaha ili wawe na amani,”
alisema Devotha.
NI LAANA NZITO?
Kwenye mazungumzo hayo na
waandishi wetu, Devotha aliendelea kutiririka kuwa kutokana Kanumba
kufariki dunia akiwa na kitu moyoni kuna uwezekano mkubwa kwamba kuna
kitu alikizungumza muda mchache kabla hajafariki au kuwa na kinyongo na
Bongo Movie hivyo wasanii hao wanatakiwa kwenda kuomba msamaha kaburini
kwake ili kundi hilo lisimame tena.
Staa katika tasnia ya filamu Bongo Dk. Cheni.
WAOMBA RADHI KIMYAKIMYA
Uchunguzi wa gazeti hili
umebaini kwamba kuna baadhi ya wasanii wamedaiwa kuanza kwenda kaburini
hapo kimyakimya na kuomba radhi ili kundi lao lirudi kwenye mstari kama
lilivyokuwa enzi za marehemu Kanumba.
“Tumeona
hali ni mbaya bora twende vinginevyo mambo yataharibika zaidi ya hapa,”
alisema msanii mwenye taito kubwa ndani ya Bongo Movie kwa sharti la
kustiriwa jina.
WENGINE KUOMBA RADHI
Ijumaa lilizungumza na
baadhi ya wasanii kwa sharti la kutotaja majina yao ambao walikiri
kwamba mambo hayaendi sawa kutokana na laana ya Kanumba hivyo wako
mbioni kwenda kuomba msamaha katika kaburi lake wakiamini uliokufa ni
mwili roho ingali hai.
KUMBUKUMBU
Marehemu Kanumba
alifariki dunia Aprili 7, 2012 nyumbani kwake, Sinza-Vatcan akiwa na
aliyekuwa mpenzi wake, Elizabeth Michael ‘Lulu’. Alizikwa katika
Makaburi ya Kinondoni jijini Dar.




