KWELI KABLA HUJAFA HAUJA UMBIKA.! MREMBO ALILIA MILIONI TANO ILI AWE KAMA ZAMANI
MSICHANA Zuhuru Juma (27) mkazi wa Temeke jijini Dar, ambaye mguu wake mmoja umevimba kiasi cha kufikisha uzito wa kilo 75 na kums...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/09/kweli-kabla-hujafa-hauja-umbika-mrembo.html
MSICHANA Zuhuru
Juma (27) mkazi wa Temeke jijini Dar, ambaye mguu wake mmoja umevimba
kiasi cha kufikisha uzito wa kilo 75 na kumsababishia maumivu makali,
anahitaji kiasi cha shilingi 5,000,000 ili aweze kufanyiwa upasuaji
nchini India.
Msichana Zuhuru Juma (27) mkazi wa Temeke jijini Dar, ambaye mguu wake mmoja umevimba kiasi cha kufikisha uzito wa kilo 75.
Uvimbe
huo unaomfanya alie kila mara uliifanya Kampuni ya Global Publishers
kwa kushirikiana na Kipindi cha Mimi na Tanzania kinachorushwa na Kituo
cha Televisheni cha DTV, kuwasiliana na daktari aitwaye Sabapathy wa
India, aliyekubali kuifanya kazi hiyo kwa kiwango hicho cha fedha,
tofauti na madai ya awali kuwa zingehitajika shilingi milioni 30.
Daktari
huyo ambaye pia alimtibia mtoto Hamisi aliyekuwa na matatizo kama hayo
ambaye hali yake inaendelea vyema, alisema msichana huyo atarejea katika
hali yake ya kawaida endapo ataweza kufika hospitalini kwake na
kumpangia kwa ajili ya upasuaji hapo Oktoba 25, mwaka huu.
Zuhura
amewaomba Watanzania kumsaidie ili kuweza kupata matatibu hayo aweze
kupona na kuendelea kuwalea watoto wake ambao ni wadogo wanaohitaji
msaada wake kama mama na kwamba aliyeguswa na tatizo linalomkabili
anaweza kumsaidia kupitia simu yake ya mkononi namba 0717319555.