KATIBU MKUU WA CCM,NDUGU KINANA ZIARANI MKOANI TANGA
http://samchardtz.blogspot.com/2014/09/katibu-mkuu-wa-ccmndugu-kinana-ziarani.html
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kulima shamba la mpunga
kwenye mradi wa kilimo kwanza wa Skimu ya Mahenge.
Mifereji ya maji kwenye shamba la skimu ya Mahenge.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishiriki kufyeka majani kwenye eneo la soko la sabasaba mjini Korogwe.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishiriki kujenga zahanati Mahenge kwa Mndolwa.
Mbunge wa Korogwe mjini Bw.
Yusuph Nassir akielezea mipango ya maendeleo ya jimbo lake wakati wa
kukagua maendeleo ya ujenzi wa zahanati ya Mahenge Kwamndolwa .
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa vyumba vya maabara vya shule ya sekondari ya Old Korogwe.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa Korogwe
kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi
Mazoezi ambapo aliwaasa vijana kuwa makini na wanasiasa wanaotanguliza
madaraka kuliko utu.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimia wakazi wa Korogwe
walifurika kwenye mkutano wa hadhara ambapo aliwaambia wananchi hao
kuchagua viongozi bora kwenye chaguzi zote zijazo,kuhakikisha watoto wao
wanaenda shule na wasirudishwe kwa sababu ya ada na mwisho
aliwasisitiza wakazi wa Korogwe kujiunga na mifuko ya Afya ya jamii.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimkaribisha Mkuu wa Wilaya ya
Korogwe Mheshimiwa Mrisho Gambo kusalimia wananchi wa Korogwe wakati wa
mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi ya
Mazoezi.
Mkuu
wa Wilaya ya Korogwe Mheshimiwa Mrisho Gambo akiwahutubia wakazi wa
Korogwe wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya
shule ya Msingi ya Mazoezi.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Korogwe
kwenye mkutano uliokuwa na umati mkubwa wa watu waliokuwa na shauku ya
kuuliza maswali kuhusu maendeleo yao ya Korogwe.
(Picha na Adam Mzee).