CHRISTIANO RONALDO AWEKA REKODI WAKATI REAL MADRID IKIENDELEZA MAUAJI LA LIGA!
http://samchardtz.blogspot.com/2014/09/christiano-ronaldo-aweka-rekodi-wakati.html
Baada
ya kuitandika Basle 5-0 katika Champions League, kisha wakaja kuifumua
Deportivo La Coruna 8 kwenye La Liga wikiendi iliyopita, jana kipigo cha
Madrid kilihamia kwa timu ya Elche katika La Liga. Wakicheza kwenye
dimba lao la Santiago Bernabeu Madrid walianza kwa kuanza kufungwa goli
na Elche kupitia mchezaji Gallego, lakini dakika chache baadae Gareth
Bale akasawazishia Madrid. Cristiano akafungua akaunti yake ya magoli
jana kwa kufunga penati katika dakika ya 28, dakika baadae akaongeza kwa
kichwa, kisha akafunga la penati tena dakika 80 kabla ya kumalizia
shughuli kwa la tano dakika ya tisini ya mchezo.
Ronaldo akaweka rekodi ya kufunga hat trick ya 25 tangu alipojiunga
na Real Madrid mwaka 2009 – huku akiisaidia Madrid kutimiza magoli 18 ya
kufunga katika mechi 3 zilizopita.
Timu zilipangwa kama ifuatavyo:
Real Madrid: Navas, Marcelo, Carvajal, Varane, Ramos, Kroos, Rodríguez, Illarramendi, Bale, Isco, Ronaldo
Subs: Casillas, Coentrão, Benzema, Hernández, Arbeloa, Nacho, Modric
Booked: Carvajal, Marcelo
Scorers: Bale 20′, Ronaldo 28′, 32′, 80′, 90′
Elche: Yagüe, Gallego, Pelegrín, Lombán, Cisma, Romero, Corominas, Rodrigues, Mosquera, Morales, Cristian de Jesus
Booked: Gallego
Scorer: Gallego 15′
Subs: Suárez, Roco, Herrera, Martín, Fajr, Pasalic, Tyton
Ref: Carlos Clos Gómez
At: 65,000