CHEKI PICHA ZA AUNT, KASSIM WANASWA WAKIWA KATIKA TAFSIRI TOFAUTI HUKO NCHINI MAREKANI
http://samchardtz.blogspot.com/2014/09/cheki-picha-za-aunt-kassim-wanaswa.html

Amani!
Wakati mumewe Sunday Demonte akidaiwa kuwa yuko mbioni kuhukumiwa
kwenda jela huko Dubai, staa wa Bongo Movies, Aunt Ezekiel Grayson
amenaswa laivu kimahaba nchini Marekani akiwa na msanii wa muziki wa
Kizazi Kipya, Kassim Mganga.
Staa
wa Bongo Movies, Aunt Ezekiel Grayson amenaswa laivu kimahaba nchini
Marekani akiwa na msanii wa muziki wa Kizazi Kipya, Kassim Mganga.
Wakati
anaondoka nchini hivi karibuni, Aunt alionekana kwenye Uwanja wa Ndege
wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar, akiwa na mwanaume ambaye
anadaiwa kuwa ni mume wa mtu, Moses Iyobo ‘Moze’.Baada ya habari hiyo
kuripotiwa na gazeti tumbo moja na hili, Ijumaa Wikienda, Septemba 15,
mwaka huu, ilidaiwa kwamba ndugu wa mumewe, Sunday hawakufurahishwa na
kitendo hicho.
Wakipata msosi.
“Tunashangaa
kumuona Aunt ameambatana na mume wa mtu na huko anakoenda pia tunasikia
watakuwa wawili tu na Kassim, inatutia shaka kwa kweli,” alisema mmoja
wa ndugu wa mume kwa sharti la kutoanika jina lake.
Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichopo nchini Marekani, wawili hao walitia maguu hivi karibuni kwa mwaliko maalum wa Ubalozi wa Tanzania nchini humo ambapo Kassim alipewa nafasi mbili hivyo akaamua kumchukua Aunt.

Msanii wa muziki wa Kizazi Kipya, Kassim Mganga.
“Kassim
aliambiwa atafute kampani ya kuja nayo huku ndipo akaona Aunt anafaa
kwa kuwa mwenyewe amedai ni mtu wake wa karibu,” kilisema chanzo hicho.
Chanzo hicho kilizidi kumwaga data kwamba, baada ya wawili hao kufika nchini humo, walipanga katika hoteli moja kisha kuanza kujiachia kwenye viwanja tofautitofauti wakila bata ndani ya Jiji la New York.

Staa wa Bongo Movies, Aunt Ezekiel Grayson.
Baada
ya mwanahabari wetu kunasa mchapo huo, alimtafuta Aunt kupitia WhatsApp
hakupatikana, bahati nzuri Kassim alipatikana na kusema:“Tumekuja kwa
mwaliko wa ubalozi wetu, Aunt ni mshkaji wangu kwa hiyo usishangae sana
nikila naye bata,” alijibu Kassim.
Bonyeza Hapa like page yetu