BRENDAN ROGERS AMEKIRI LIVERPOOL KUSHUKA KWA KUMKOSA LUIS SUAREZ…
http://samchardtz.blogspot.com/2014/09/brendan-rogers-amekiri-liverpool.html
Kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers akielekeza wachezaji wake katika mazoezi yaliyofanyika jana uwanja wa Melwood
BRENDAN Rodgers amekiri kuwa Liverpool kwa kiasi fulani imevunjika baada ya kuondoka kwa Luis Suarez majira ya kiangazi mwaka huu.
Bosi huyo wa Liverpool amesema ushindi katika mechi ya watani wa jadi wa Merseyside kesho dhidi ya Everton itakuwa mwanzo mpya wa ligi msimu huu.
Majogoo hao katika dirisha la majira ya kiangazi mwaka huu walisajili wachezaji tisa na kumuuza Suarez kwenda Barcelona, lakini wameshindwa kuonesha makali yao.
Liverpool wamepoteza mechi tatu kati ya tano walizocheza za ligi kuu England na tatizo kubwa limetokana na uwezo mdogo wa kujilinda, lakini Rodgers amekiri kuwa ubora wao wa msimu ulipoita umepungua sana.
Liverpool wanamkosa mshambuliaji hatari Luis Suarez (juu) ambaye aliuzwa Barcelona kwa dau la paundi milioni 75 majira ya kiangazi mwaka huu.