BONGO MUVI INAKUFA..CATHY AFUNGUKA YA MOYONI!
http://samchardtz.blogspot.com/2014/09/bongo-muvi-inakufacathy-afunguka-ya.html

MSANII wa filamu ambaye pia ni mweka hazina msaidizi wa klabu ya
Bongo Movie Unity, Sabrina Rupia ‘Cathy’ amefunguka kwamba anaona kundi
hilo linakwenda kufa na halitakuwepo kabisa kutokana na kujiuzulu kwa
mwenyekiti wao, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’
“Steve yeye kama binadamu ana mapungufu kidogo lakini mazuri
aliyofanya ni mengi kwani alikuwa mpenda maendeleo lakini kujiuzulu
kwake ni pigo na ninaona kama kundi hili halitakuwepo tena, yaani
ninajisikia vibaya sana na amejiuzulu ghafla mno,”alisema Cathy