Flatnews

Amanda Azua Balaa Mtaani Baada ya Kuvaa Nguo Fupi , Masela Wamfuata Nyuma na Kumpigia Miluzi


Msanii wa filamu, Tamrina Posh ‘Amanda’ hivi karibuni alizua balaa la aina yake baada ya kukatiza mtaani akiwa amevaa kigauni kilichokaribia kuacha wazi makalio yake.

Tukio hilo lililowashangaza wengi lilijiri eneo la Mwenge Bamaga jijini Dar wakati msanii huyo alipokuwa akitembea kuelekea kwenye mgahawa uliopo eneo hilo.


Huku akitembea kwa staili ya ‘hamsini…mia…hamsini…mia…’, Amanda alionekana kufanya makusudi kwani kadiri wanaume walivyokuwa wakijikusanya kumshangaa, ndivyo alivyoongeza mikogo na kuwaacha miudenda ikiwatoka.
Kutokana na hali hiyo, baadhi ya wanaume ambao wengi wao ni madereva wa Bajaj na mafundi gereji walionekana kumzodoa huku wakieleza kuwa, ni msanii asiyejiheshimu.
“Yule kutuvalia sisi vile ndiyo nini? Mavazi yale yanavaliwa klabu usiku tena wanaovaa vile ni wale wasioithamini miili yao, tukisema anatutangazia biashara tutakuwa tunakosea?” alihoji fundi mmoja aliyefahamika kwa jina la Juma.

Katika kujua sababu ya kuvaa kigauni hicho, mwandishi wetu alimfuata Amanda lakini kabla ya kuulizwa chochote aliingia kwenye gari na kuondoka zake baada ya kuwachimba mkwara waliokuwa wakimpigia miluzi. Baadaye alipopigiwa, simu iliita bila kupokelewa.
GPL

Post a Comment

emo-but-icon

item