WAZIRI MKUU MSTAAFU FREDRICK SUMAYE AZINDUA ALBAM YA "SHIKILIA PINDO LA YESU" YA ROSE MUHANDO DIAMOND
http://samchardtz.blogspot.com/2014/08/waziri-mkuu-mstaafu-fredrick-sumaye.html
Waziri
Mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye akikata utepe wakati akizindua rasmi
albam ya Rose Muhando mwimbaji wa muziki wa injili inayoitwa Shikilia
Pindo la Yesu katika onesho kubwa la uzinduzi lililofanyika kwenye
ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam leo likihudhuriwa na
maelefu ya washabiki wa muziki wa injili, ambapo waimbaji mbalimbali
wameshiriki katika uzinduzi huo wakiwemo Ephraim Sekereti Kutoka Zambia,
Sara K. kutoka Kenya , Upendo Kilahiro, Upendo Nkone John Lisu na
wengine wengi, Katika uzinduzi huo pia maaskofu na wachungaji kutoka
makanisa mbalimbali wamehudhuria, Katikati anayeshirikiana na Mh.
Fredrick Sumaye ni Alex Msama Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion
iliyoandaa uzinduzi huo na kushoto ni Mwimbaji Rose Muhando mwenyewe.

Waziri Mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye akionyesha Juu albam ya Shikilia Pindo la Yesu ya Rose Muhando mara baada ya kuizindua rasmi kulia ni Alex Msama Mkurugenzi wa Msama Promotion.

Waziri
Mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye akimsikiliza Askofu Mwakibolwa wa
makanisa ya Pentekosti akimkaribisha Mgeni rasmi Waziri Mkuu mstaafu Mh.
Fredric Sumaye ili kuzungumza na waalikwa na washabiki mbalimbali wa
muziki wa injili.

Waziri
Mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye akisoma hotuba yake wakati alipozindua
albam ya mwimbaji wa muziki wa injili Rose Muhando leo kwenye ukumbi wa
Diamond Jubilee.

Rose
Muhando mwimbaji wa muziki wa injili akishirikiana na waimbaji wake
wakati wa uzinduzi wa albam yae ya Shikilia Pindo la Yesu leo kwenye
ukumbi wa Diamond Jubilee.

Rose
Muhando mwimbaji wa muziki wa injili akifanya vitu vyake wakati wa
uzinduzi wa albam yake ya Shikilia Pindo la Yesu jijini Dar es salaam
leo

Mashabiki mbalimbali wakiwa wamefurika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.

Mashabiki mbalimbali wakiwa wamefurika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee

Mwimbaji Upendo Kilahiro akiwa amekaa na Emmanuel Mbasha wakati wa uzinduzi wa Albam ya Rose Mundo ya Shikilia Pindo la Yesu.

Waimbaji wa mwimbaji Rose Muhando wakiwajibika jukwaani

Mwimbaji Sara K kutoka nchini Kenya aifanya vitu vyake jukwaani.

Upendo Nkone akikamua na Mumewe jukwaani ambaye alimtambulisha bila kumtaja jina kama wanavyoonekana.

Mwimbaji Jhn Lisu akifanya vitu vyake

Mwimbaji Upendo Kilahiro akiwa amekaa na Emmanuel Mbasha

Mgeni
Rami Mh. Fredrick Sumaye wa pili kutoka kushoto pamoja na wageni wa
meza kuu wakifurahia muziki wa injili utoka kwa mwimbaji Rose Muhando
hayupo pichani.

Mwimbaji Ephraim Sekereti kutoka nchini Zambia akikamua mble ya wageni waalikwa

Mgeni Rami Mh. Fredrick Sumaye akimpongeza mwimbaji Rose Muhando mara baada ya kuzindua albam yake ya Shikilia Pindo la Yesu.

Mgeni Rami Mh. Fredrick Sumaye akiteta jambo na MC Mwakipesile aliyeongoza shughuli hiyo wakati wa onesho hilo la uzinduzi
