TFF MNAZIKUMBUKA BUSARA ZA KIM NA JAM POULSEN?, TUSIPORUDI HUKU…MAJANGA KWENDA MBELE! Kitaifa , Makala ...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/08/tff-mnazikumbuka-busara-za-kim-na-jam.html
TFF MNAZIKUMBUKA BUSARA ZA KIM NA JAM POULSEN?, TUSIPORUDI HUKU…MAJANGA KWENDA MBELE! Kitaifa, Makala
Jan Poulsen alirithi mikoba ya Mbrazil Marcio Maximo kuifundisha timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars mwaka 2010
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
0712461976
TAIFA Stars imekuwa timu ya ‘Tia maji Tia maji’ kwa miaka mingi, lakini kwasasa kuna haja ya kuanza upya kuijenga timu hii.
Kumbukumbu: mwaka 1980 Stars ilishiriki fainali za mataifa ya Afrika zilizofanyika nchini Nigeria.
Kuanzia hapo mpaka leo hii, imekuwa ndoto ya mchana kwasababu ya mipango mibovu katika soka la Tanzania.
Mwaka 2009, Stars ilishiriki
mashindano mengine makubwa ya mataifa ya Africa kwa wachezaji wanaocheza
ligi za ndani, CHAN, nchini Ivory Coast.
Wakati inakwenda Ivory, Stars
chini ya kocha Mbrazil, Marcio Maximo ilionekana kufufuka na kulikuwa na
morali kubwa kwa wachezaji, viongozi na mashabiki kwa ujumla.
Baada ya kuondoka kwa Maximo
mwaka 2010, TFF ilimteua Mdenish Jan Poulsen. Mzee huyu alikuwa na
mipango mizuri, lakini ilionekana kushindikana kutokana na uharaka wa
Watanzania.
Ni kweli Stars ilishuka kiwango
ukilinganisha na kipindi cha Maximo, lakini Jan alikuwa na mipango ya
muda mrefu, jambo ambalo ni adui wa Watanzania wengi.
Njia za mkato zinapenda kweli, eti leo hii mtu anatafakari kufuzu kombe la dunia au Afcon 2015, kwa mipango ipi?
Siku moja wakati anatoa kozi kwa makocha wa Tanzania alichora mchoro katika ubao.
Wote walioenda shule wanajua mbao za kuandikia wakati walimu wanafundisha zilivyo. Rudisha kumbukumbu.
Jan aliandika pointi A chini kabisa ya ubao na akaandika pointi B juu kabisa ya ubao.
Akasema Tanzania ipo pointi A
ambapo soka la Tanzania lipo. Hicho ni kiwango cha chini kabisa, lakini
soka hilo linatakiwa kufikia pointi B, ngazi au kiwango ya juu kabisa.
Mdenish huyo aliuliza swali,
tunafikaje pointi B?. Akafafanua kuwa ili kufika pointi B, hapa katikati
kuna kitu kinaitwa mchakato ‘Process’.
Kim Poulsen alirithi mikoba ya Mdenish mwenzake, Jan Poulsen kuinoa Taifa Stars
Huu mchakato unajumuisha kuandaa mipango sahihi, mfumo sahihi wa soka, hususani soka la vijana.
Jan alieleza kuwa ili kufanikiwa
kufika Pointi B, lazima kuwekeza muda na fedha za kutosha kuandaa timu
za vijana, miundo mbinu ya soka, kuandaa makocha wenye ueledi wa juu na
kuwa na viongozi sahihi katika nafasi sahihi.
Wakati anayasema hayo, alionekana
kugundua matatizo ya wachezaji wa Tanzania. Alipoondoka na kumuachia
Kim Poulsen, mambo yalionekana kuwa poa, lakini ghafla watu wakasitisha
programu za kim na kumleta Mart Nooij.
Siku Kim anaaga pala TFF,
aliongea vitu vingi, lakini nilishika zaidi kitu alichosema ‘Things
Takes Time’ (TTT). Hapa kocha huyu alimaanisha vitu vinahitaji muda.
Soka linahitaji muda.
Lazima kuwa na uvumilivu
unapojenga timu. Kwa maana yake yeye, Kim alikuwa anajenga timu na
alikuwa na program ya muda mrefu hasa katika soka la vijana, lakini
kutokana na uchu wa kutaka kufuzu AFCON 2015 akamtimuliwa.
Viongozi wa juu wa TFF
walikaririwa mara kadhaa wakisema kwa vyovyote vile, kwa kumwaga damu
uwanjani, lazima Taifa Stars iende AFCON 2015.
Tayari Kim alisema mapema kuwa
malengo yake yalikuwa AFCON 2015 nchini Morocco na sio kombe la dunia
2014 au CECAFA Senior Challenge Cup 2014 nchini Kenya, lakini watu
wakata mafanikio ya haraka haraka.
Mpira haulazimishwi. Lazima mipango sahihi iweke na uvumilivu uwepo.
Busara za Kim na Jan Poulsen si
za kuziacha hata kidogo. Walikuwa na maana kubwa, tena ile ile aliyonayo
Mart Nooij. Sema namna viongozi wanavyochukuliwa mambo kwa haraka ndio
matokeo ya kule Msumbiji mwishoni mwa wiki iliyopita.
TFF wamekuwa wakijitahidi
kuiandaa timu, kwa mfano mwaka huu waliweka kambi Botswana kuiwinda
Msumbiji na kufanya mpango wa maboresho ya Taifa Stars ingawa kwa
asilimia 500 ‘umefeli’.
Lakini tatizo ni lile lile na
viongozi wanalijua kuwa aina ya wachezaji waliopo sasa wamekosa vitu
vingi vya kimbinu na kiufundi kwasababu wengi wao walikosa misingi ya
mpira enzi za utoto wao.
Nadhini ni lazima turudi nyuma na kuwekeza katika soka la vijana.
Unajua kwa mara ya kwanza nafasi
nzuri zaidi ambayo Tanzania ilishika katika viwango vya FIFA? Hii ni
mwaka 1965 ambapo ilishika nafasi ya 65.
Wachezaji wengi wa timu ya 1965 ndio walioipeleka Taifa Stars michuano ya mataifa ya Afrika 1980 nchini Morocco.
Asubuhi njema!
