S.Leone yapiga marufuku Kandanda
http://samchardtz.blogspot.com/2014/08/sleone-yapiga-marufuku-kandanda.html
Shirikisho la soka la Sierra
Leone limepiga marufuku mechi zote za kandanda nchini humo ikihofia
kuenea zaidi kwa maradhi ya homa ya Ebola.
Hatua hiyo inafuatia marufuku iliyotangazwa na
rais Ernest Bai Koroma katika jitihada za kuzuia kuenea zaidi kwa
maradhi ya ebola nchini humo.Hali hiyo ya tahadhari iliyotangazwa na rais inatarajiwa kudumu kwa kipindi cha siku 60 hadi 90.

S.Leone ilikuwa inatarajiwa kuikaribisha Cameroon mwezi ujao
Aidha maandalizi ya mechi ya ufunguzi ya kundi D dhidi ya Ivory Coast inatarajiwa pia kuathirika.
Marufuku hiyo pia itaathiri pakubwa maandalizi na mechi za mkondo wa pili wa ligi ya Sierra Leone.

Maambukizi ya ugonjwa wa Ebola Magharibi mwa Afrika
Makataa hiyo iliifaidi timu ya Sierra Leone ambayo ilijizolea alama tatu bila hata kutoa kijasho.
