Michezo ya Jumuiya ya Madola yafikia tamati
http://samchardtz.blogspot.com/2014/08/michezo-ya-jumuiya-ya-madola-yafikia.html
Mji wa Glasgow umesherehekea kumalizika kwa Michezo ya Jumuiya ya Madola
katika tamasha la kipekee, huku waandalizi wakiwapongeza washiriki kwa
kile walichokiita kuwa ni “Michezo ya Kirafiki”.
Bendera ya Michezo ya Jumuiya ya Madola ilikabidhiwa maafisa wa Australia ambao ndio watakaoandaa michezo ijayo mwaka wa 2018, katika mji wa Gold Coast, wa jimbo la kaskazini mashariki la Queensland.
Na hata wakati ikikabidhiwa bendera, Australia iliondolewa kileleni mwa msimamo wa medali kwa mara ya kwanza tangu mwaka wa 1986. England ilinyakua nafasi ya kwanza ikiwa na dhahabu 58, ikifuatwa na Australia katika nafasi ya pili na dhahabu 49. Canada ilikuwa ya tatu na 32 wakati Scotland ikimaliza ya nne na 19.
