Shambulio la Israel laua wapalestna 10
http://samchardtz.blogspot.com/2014/08/shambulio-la-israel-laua-wapalestna-10.html
Baadhi ya majeruhi katika shambulio hilo wakipatiwa huduma ya kwanza.
Mpalestina
huyu akijaribu kuokoa maisha ya mtoto baada ya kushambuliwa na Israel
leo.WATU 10 wamepoteza maisha huku 35 wakijeruhiwa baada ya shambulio la
angani la Israel leo katika shule moja ya Umoja wa Mataifa iliyopo
katika mji wa Rafah, Palestina.Walioshuhudia shambulio hilo wanasema
kuwa kombora lilipiga karibu na mlango wa shule hiyo. Kati ya
waliofariki ni watoto na wanawake waliokuwa kwenye foleni kwa ajili ya
kuchukua chakula.Leo ni siku ya 27 tangu mapigano hayo makali kati ya
Israel na Palestina kuanza ambapo jumla ya Wapalestina 1,700 na Waisrael
67 wamepoteza maisha mpaka sasa.Shambulio hili limetokea baada ya siku
nne tangu shambulio ligine kuua Wapalestina 15 waliokuwa katika shule ya
Umoja wa Mataifa iliyopo Jabalya.


Baadhi ya Wapalestina wakilaani mashambulio yanayofanywa na Israel nchini huo huku miili na majeruhi ikiwa chini.

Majeruhi wakizidi kupatiwa huduma ya kwanza.
