NCCR-Mageuzi kuipeleka IPTL kwa wananchi
http://samchardtz.blogspot.com/2014/08/nccr-mageuzi-kuipeleka-iptl-kwa-wananchi.html
CHAMA cha NCCR Mageuzi kimetangaza kulipeleka sakata la IPTL kwa wananchi na kutoa elimu kwao namna suala hilo lilivyozimwa na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Chama hicho kimesema kinatarajia kuanza ziara mkoani Kigoma wiki ijayo, huku ajenda kubwa ikiwa ni sakata la IPTL.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Mosen
Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila
“Hatujaridhishwa na hatua zinazochukuliwa na Serikali juu ya suala hili, hivyo tunafanya utaratibu wa kuwasiliana na vyama ndani ya Ukawa kuona namna bora ya kulisukuma suala hili, ili Watanzania waelewe jinsi nchi yao inavyotafunwa.
“Pia tunaviomba hata vyama vilivyo nje ya Ukawa kulitambua suala hili na kulichukulia ni la wote na si la Kafulila au NCCR peke yake. Tunaamini fedha zilizochotwa kwenye akaunti ya Escrow zinalengwa kutumika kwenye harakati za uchaguzi mkuu ujao,” alisema Nyambabe.
Katibu Mkuu huyo wa NCCR-Mageuzi alisema kutokana na uzito unaochukuliwa sasa, hakuna dalili ya jambo hilo kupewa umuhimu, licha ya kuamuliwa lichunguzwe na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Fedha za Serikali (CAG) na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).
Alisema ukweli kuhusu suala hilo, Spika wa Bunge, Anne Makinda alitakiwa kuunda kamati teule ambayo ingeweza kutoa majibu ya kweli kuhusu wizi huo.
“Ni aibu kwa Spika kukataa Bunge lisichukue jukumu lake la kuichunguza Serikali. Wote tunafahamu CAG alivyomsafisha Jairo au Takukuru ilivyosafisha Richmond.
“Ni katika msingi huo kama chama tunashauri suala hili linalogusa vigogo wakubwa nchini lichunguzwe na Bunge lenyewe au uchunguzi ufanywe na kampuni za kimataifa za ukaguzi kama ilivyofanyika kwenye fedha za EPA,” alisema.
Akizungumzia suala la usalama wa Kafulila, alisema endapo jambo lolote baya litamtokea mbunge huyo, NCCR Mageuzi inajua wanaohusika ni baadhi ya watendaji wa Serikali ambao wamekuwa wakitoa vitisho kila kukicha kwa mbunge huyo.
Kwa upande wake, Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila, alisema katu hatorudi nyuma licha ya kupokea vitisho.
“Sitaogopa lolote, nitaendelea kusema kweli na sasa ninaandika kitabu kitakachoeleza ufisadi huu na ninamuomba Mungu kabla kichwa hakijakatwa niwe nimekimaliza,” alisema Kafulila.
Juni 26, mwaka huu, Kafulila aliingia katika mapambano na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema, ambaye alimfananisha mbunge huyo na tumbili.
Kutokana na kauli hiyo, naye Kafulila alijibu mapigo kwa kumwita Jaji Werema mwizi kwa kumtaka atangaze maslahi katika sakata la uchotwaji wa Sh bilioni 200 katika akaunti ya Escrow.
