Mashambulizi Gaza yasitishwa kwa masaa 72
http://samchardtz.blogspot.com/2014/08/mashambulizi-gaza-yasitishwa-kwa-masaa_5.html
Israel inasema imeondowa wanajeshi wake wote wa ardhini kutoka Gaza baada ya kukamilisha operesheni yake iliyoanza katikati ya mwezi uliopita, huku muda wa usitishaji mapigano kwa muda wa siku tatu ukianza.
Wanajeshi wa Israel wakiondoka kutoka Ukanda wa Gaza usiku wa tarehe 5 Agosti 2014.
Msemaji wa jeshi la Israel, Jenerali Moti Almoz, amekiambia kituo cha
redio ya jeshi hilo asubuhi ya leo kwamba kulikuwa na wanajeshi kadhaa
ndani ya Gaza, lakini kwa sasa wote wameondoka.Mashahidi wanasema wanajeshi hao wa ardhini walianza kuondoka alfajiri ya leo, muda mchache kabla ya kuanza kwa masaa 72 ya ya kusitisha mapigano ambao ulianza saa 2 asubuhi kwa majira ya Mashariki ya Kati.
Hata hivyo, Luteni Kanali Peter Lerner wa jeshi la Israel, amesema wanajeshi watawekwa kwenye maeneo ya kujilinda nje ya Gaza, na kwamba watajibu endapo watashambuliwa.
Kwa upande mwengine, ripoti zinasema usiku wa kuamkia leo, maroketi kutoka upande wa Gaza yaliangukia Israel, katika kile Hamas ilichosema ni kulipiza kisasi "mauaji ya maangamizi". Milio ya hadhari ilisikika kaskazini mwa mji wa Jerusalem, lakini hakuna taarifa yoyote ya watu waliouawa ama kujeruhiwa.
Roketi moja liliangukia karibu na nyumba moja mjini Bait-Lahm kwenye Ukingo wa Magharibi. Mkaazi mmoja wa nyumba hiyo, Elias Jubran, ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba walisikia mshindo mkubwa usiku wa kuamkia leo, ambapo madirisha na milango ya nyumba kadhaa za eneo hilo ilivunjika, ingawa hakuna mtu aliyejeruhiwa wala kuuawa.
Waziri ajiuzulu Uingereza
Wananchi wa Misri wakiandamana mjini Cairo kuwaunga mkono Wapalestina kwenye Ukanda wa Gaza katikati ya mwezi Machi 2014.Kufikia sasa, mashambulizi haya ya takribani mwezi mmoja dhidi ya Gaza yamesababisha vifo vya Wapalestina 1,834 na huku Israel ikipoteza wanajeshi 64 na raia watatu.
Mbali na hasara hiyo ya maisha ya watu, pande zote mbili zimehasirika sana kiuchumi. Gaza inakabiliwa na ujenzi mpya wa makaazi na miundo mbinu utakaogharimu dola bilioni 6, huku Israel ikipoteza mamilioni ya dola kwenye sekta za utalii na viwanda.
