KAMPUNI YA NDEGE YA FASTJET YAZINDUA SAFARI ZAKE KATI YA (DAR – HARARE-DAR) USIKU HUU MJINI HARARE
http://samchardtz.blogspot.com/2014/08/kampuni-ya-ndege-ya-fastjet-yazindua_5.html
Waziri
wa Usafirishaji wa Zimbabwe Dr. Orbet Mpofu wa tatu kutoka kulia na
Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe Balozi Adadi Rajabu wa tatu kutoka
kushoto wakiwa pamoja na baadhi ya viongozi wa serikali ya Zimbabwe na
wakuu wa kampuni ya Fastjet wakati wa uzinduzi wa safari za ndege za
kampuni hiyo kati ya Tanzania na Zimbabwe unaofanyika usiku huu kwenye
uwanja wa ndege wa Harare Fullshangwe Inakuletea matukio haya moja kwa
moja kutoka Zimbabwe Harare usiku huu. PICHA NA KIKOSIKAZI CHA
FULLSHANGWE-HARARE – ZIMBABWE.
Baadhi
ya wafanyakazi wa kampuni ya ndege ya Fastjet wakipeperusha bendera ya
Zimbabwe mara baada ya ndege hiyo kutua kwenye uwanja wa ndege wa Harare
kwa mara ya kwanza nchini Zimbabwe.
Balozi
mdogo wa Zimbabwe nchini Tanzania Balozi Walter Sande akisalimiana na
Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe Balozi Adadi Rajabu mara baada ya
kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Harare usiku huu.
Meneja
Masoko wa Bodi ya Utalii Geofrey Meena kulia na Mkuu wa Kitengo cha
mawasiliano bodi ya utalii Geofrey Tengeneza katikati wakisalimiana na
wenyeji wao mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Harare
wakiwa ni miongoni mwa abiria waliosafiri na ndege ya Fastjet wakati wa
uzinduzi wa safari zake katika ya Tanzania na Zimbabwe leo.
Viongozi
wa serikali ya Zimbabwe na Tanzania pamoja na wakuu wa kampuni ya
Fastjet wakipiga picha ya pamoja mbele ya ndege ya Fastjet mara baada ya
ndege hiyo kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Harare.
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika hafla hiyo usiku huu
Wageni waalikwa mbalimbali wakiwa katika hafla hiyo inayoendeea usiku huu.
Mwanamuziki
Tariro Chaniwa wa nchini Zimbabwe akiimba nyimbo za taifa za Zimbabwe
na Tanzania wakati wa ufunguzi wa hafla hiyo ya uzinduzi wa safari za
kampuni ya ndege ya Fastjet.
Ndege ya Fastjet ikiwa imeegeshwa katika uwanja wa ndege wa wa kimataifa wa Harare nchini Zimbabwe.








