Mchezaji nyota wa kimataifa wa Holland na Ajax, Daley Blind.
http://samchardtz.blogspot.com/2014/08/manchester-united-kumsajili-beki-kitasa.html

Mchezaji nyota wa kimataifa wa Holland na Ajax, Daley Blind.
MANCHESTER UNITED imekubali kulipa dau la pauni milioni 14.2 iliyohitajiwa na Ajax ili kumsajili nyota wa kimataifa wa Holland Daley Blind.Kilichobakia
sasa kwa Blind mwenye umri wa miaka 24 ni kukubaliana na United kuhusu
maslahi yake binafsi na kwenda kufanya vipimo vya afya.United
inaamini mchezaji huyo mwenye uwezo wa kucheza kama beki wa kushoto,
beki wa kati na kiungo mkabaji, atakamilisha usajili wake kabla dirisha
la usajil halijafungwa.
Habari
kutoka Holland zinasema ada iliyofikiwa ni pauni 14.2 ambapo United
ikathibitisha kupitia akaunti yake ya Twitter kuwa wamekubaliana na ada
hiyo na watatangaza kitakachojiri hapo baadae.