MANCHESTER CITY WAJIBU HOJA YA MFARANSA ASERNE WENGER
http://samchardtz.blogspot.com/2014/08/manchester-city-wajibu-hoja-ya-mfaransa.html
Wanajiamini: Man City hawaamini kama wamevunja sheria ya matumizi ya fedha baada ya kumsajili Lampard kwa mkopo.
MANCHESTER City wanajiamini kuwa hawajavunja sheria ya matumizi ya fedha baada ya kumchukua kwa mkopo Frank James Lampard.
Kiungo huyo mwenye miaka 36 alisaini
miaka miwili kuitumikia klabu ya New York City-moja ya klabu
inayomilikiwa na Manchester City.
Lakini timu hiyo ya Marekani haitacheza
ligi mpaka mwezi wa tatu mwakani, kwahiyo Lampard atacheza ligi kuu
nchini England kwa mkopo mpaka januari mwakani.
Mkataba mpya: Kiungo huyu alijiunga na New York FC kwa mkatana wa miaka miwili baada ya kuachiwa na Chelsea.
Kocha wa Asernal, Mfaransa Aserne Wenger
aliibua wasiwasi mwishoni mwa wiki alipohoji kama mkataba wa mkopo wa
Lampard upo sahihi na umeendana na sheria ya matumizi ya fedha (FFP)
ambayo inaitaka klabu kutotumia fedha nyingi kuliko mapato yake.
Man City walishindwa kufuata sheria ya
UEFA ya matumizi ya fedha msimu uliopita na sasa wanatakiwa kujumuisha
wachezaji watano wazawa katika kikosi cha wachezaji 21 kitakachoshiriki
UEFA msimu ujao ampao Lampard atakuwa miongoni mwao.
Hata hivyo, City ambao wanakaribia
kuvunja tena sheria mwaka huu, wanaamini kwamba hawajavunja sheria ya
matumizi ya fedha ya UEFA baada ya kumsajili Lampard.
Sheria za UEFA zinaelezea kuwa mkataba
wa mkopo wa Lampard unaingia katika sheria ya matumizi ya fedha
kwasababu Man city watakuwa wanamlipa posho kiungo huyo wa zamani wa
Chelsea.
Arsene Wenger ameibuka wasiwasi kuhusiana na dili la Lampard
