ATUMIA MLEMAVU WAKE WA MGUU BANDIA KUUZA DAWA ZA KULEVYA
http://samchardtz.blogspot.com/2014/08/atumia-mlemavu-wake-wa-mguu-bandia.html
Kamishna Kova akiwa na RPC mpya wa Temeke, Kihenya Kihenya.
Kamishna Kova akiwa kashika moja ya dawa ya kulevya huku afande Alfred akiwa kashika mguu huo wa bandia anaotumia mlemavu.
Kamishna Suleiman Kova akionesha namna mguu huo wa mtu mwenye ulemavu unavyotumika kutunzia dawa za kulevya.
KIJANA mmoja ambaye ni mlemavu wa mguu,
Said Tindwa (36), mkazi wa Vijibweni Kigamboni jijini Dar, anashikiliwa
na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kutumia mguu wake
wa bandia kwa ajili ya kutunzia na kuuza dawa za kulevya.
Akizungumza na waandishi wa habari,
Kamishna wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum, Suleiman Kova alisema mlemavu
huyo alitiwa nguvuni Agosti 1 mwaka huu kufuatia mtego uliowekwa na
jeshi hilo.
Alisema uchunguzi wa awali unaonesha kuwa
mtuhumiwa huyo amekuwa akitumia mbinu ya kuziuza dawa hizo kwa kuzificha
kwenye mguu wake wa bandia.
Aidha Kova alisema kuwa dawa alizokuwa
akiziuza mlemavu huyo ni zile za viwandani kama vile cocaine, heroin na
wakati mwingine bangi.
“Katika mtego maalum uliowekwa na askari wa
upelelezi ndipo mlemavu huyo alikamatwa akiuza dawa hizo kwa wateja
wake baada ya kuzitoa alikozificha ambapo ni ndani ya mguu huo wa
bandia” alisema Kova.
(Na Gabriel Ng’osha/GPL)