MAMA SALMA KIKWETE AKUTANA NA WANAWAKE WATANZANIA WAJASIRIAMALI WAISHIO WASHINGTON
http://samchardtz.blogspot.com/2014/08/mama-salma-kikwete-akutana-na-wanawake.html
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea shada la maua kutoka kwa Ndugu
Juster Mutakyawa mara baada ya kuwasili kwenye ofisi ya ubalozi wa
Tanzania nchini Marekani iliyoko Washington tarehe 3.8.2014.
Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama
Salma Kikwete akipokewa na Mwenyekiti wa kikundi cha wanawake
wajasiriamali cha Watanzania wanaoishi Washington kiitwacho TANO Ladies
Ndugu Asha Hariz wakati alipotembelea ofisi ya ubalozi wa Tanzania
nchini Marekani tarehe 3.8.2014
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea kipeperushi kutoka kwa Rais na
Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Help for Underserved Communities (HUC) ya
nchini Marekani Ndugu Zawadi Sakapalla baada ya kupata taarifa ya huduma
mbalimbali zitolewazo na kampuni hiyo. Kampuni hiyo husaidia familia
maskini kwa kuwapatia huduma ya maji safi na salama kwa kuwachimbia
visima pamoja na kutoa vifaa vya elimu kwa wanafunzi.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na akina mama wa kitanzania
wajasiriamali wanaoishi nchini Marekani kwenye ukumbi wa ofisi ya
ubalozi wetu mjini Washington tarehe 3.8.2014.
Baadhi
ya wanawake wajasiriamali na wafanyakazi wa ubalozi wa Tanzania nchini
Marekani wakisikiliza kwa makini hotuba iliyokuwa ikitolewa na Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete.
PICHA NA JOHN LUKUWI.