HULL KUCHUANA NA LOKEREN YA UBELGIJI, TOTTENHAM USO KWA USO NA AEL LIMASSOL YA CYPRIOT LIGI YA EUROPA
Mkombozi: Sone Aluko aliifungia goli pekee la ushindi klabu ya Hull City dhidi ya AS Trencin.
http://samchardtz.blogspot.com/2014/08/hull-kuchuana-na-lokeren-ya-ubelgiji.html

HULL itachuana na Lokeren katika mechi mbili za raundi ya pili ya mtoano ya ligi ya Europa.
Kikosi hicho cha Steve Bruce kiliitandika AS Trencin ya Slovakia kwa wastani wa mabao 2-1 katika mchezo wa jana alhamisi na sasa watakabiliana na timu hiyo ya Ubelgiji.
Wakati huo huo, Tottenham watakabiliana na timu ya Cypriot ya AEL Limassol, ambao wapo katika mashindano hayo baada ya kupoteza mechi kwa mabao 3-1 dhidi ya timu ya Zenit Saint Petersburg chini ya Andre Villas-Boas katika mchezo wa raundi ya tatu ya kufuzu UEFA.
DROO NZIMA YA EUROPA
EUROPA LEAGUE PLAY-OFF ROUND DRAW