WAZIRI WA FEDHA SAADA MKUYA SALUM AKIWASILISHA BAJETI YA SERIKALI
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/waziri-wa-fedha-saada-mkuya-salum.html
Waziri
wa Fedha Saada Mkuya Salum akiwasili Bungeni alipokuwa anaenda
kuwasilisha hotuba ya mapendekezo ya Bajeti ya Serikali kuhusu makadirio
ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2014/2015 leo mjini Dodoma.
Waziri
wa Fedha Saada Mkuya Salum akiwasilisha hotuba ya mapendekezo ya
Serikali kuhusu makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha
2014/2015 leo Bungeni mjini Dodoma. Waliokaa viti vya nyuma ni Manaibu
Waziri wa wizara ya Fedha kushoto ni Mwigulu Nchemba na kulia ni Adam
Malima.
Baadhi
ya Wabunge wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum
alipokuwa anawasilisha mapendekezo ya Bajeti ya Serikali kuhusu
makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2014/2015 leo
Bungeni mjini Dodoma.
Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha Dk. Servacius Likwalile (wa tatu kushoto mstari wa
pili kutoka nyuma), Maafisa wakuu wa Serikali na baadhi ya wageni
waalikwa wakifuatilia kwa makini hotuba ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka
wa fedha 2014/2015 leo Bungeni mjini Dodoma.
Washirika wa Maendeleo nchini wakifuatilia hotuba iliyowasilishwa na Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum ya mapendekezo ya Bajeti ya Serikali kuhusu makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2014/2015 leo Bungeni mjini Dodoma.