Flatnews

Wasunni wateka Anbar, Magharibi mwa Iraq


Wapiganaji wa Isis wakifanya gwaride
Wanamgambo wa Kisuni nchini Iraq wamechukuwa uthibiti kamili wa mipaka yote ya taifa hilo na mataifa ya Syria na Jordan baada ya kuteka maeneo mawili ya mwisho ya vivuko vya mpakani katika mkoa wa magharibi wa Anbar nchini Iraq.

Maafisa wa usalama wamesema kuwa waasi hao wanaoongozwa na kundi la wanamgambo wa madhehebu ya kiislamu wa Kisunni maarufu kama ISIS wameteka eneo la al-Waleed lililopo karibu na mpaka wa Syria na mji wa Turaibil uliopo njiani kuelekea nchini Jordan.
Mapema Jumapili wanamgambo hao waliteka miji mingine mitatu Magharibi mwa nchi hiyo.
Serikali ilisema kuwa katika maeneo fulani, wanajeshi wameondoka kimpango. Mwanachama Msuni maarufu nchini, Shaikh Raad al-Suleiman, kutoka Ramadi, alisema kuwa ni idadi ndogo tu ya wanachama wa ISIS wameingia katika Mkoa wa Anbar.
"Ndio kuna wanachama wachache wa Isis ambao wameingia katika Mkoa wa Anbar, wachache sana, hawazidi asilimia tano, lakini inaonekana wanachama wa Al Qaida na wakaazi wa vijiji hivyo wenye itikadi kali wanashirikiana. Ushirikiano unaotakana na haja ya wanavijiji kutaka kujilinda," al-Suleiman alisema.
Awali katika mahojiano kwenye kipindi cha televisheni cha CBS Face the Nation, Rais Obama alieleza hatari inayoweza kuletwa na kundi la wapiganaji la ISIS. Alisema kundi hilo ni hatari ya muda mrefu kwa Marekani na huenda kundi hilo likatenganisha wakaazi wa maeneo yote waliyoteka kutoka kwa maeneo mengine ya dunia.
"Msimamo wao mkali unatishia usalama wa sasa na wa muda mrefu ujao. Kuna makundi mengine kule nje ambayo pengine yana mipango hatari zaidi ya wakati huu inayolenga Marekani ambayo lazima sisi kama Marekani tujitahadhari nayo
Ukweli wa kundi kama hili ni kuwa kwa kawaida linapoteka eneo fulani, kwa sababu wao huwa wakatili, kwa sababu wana misamamo mikali, baada ya muda fulani wakaazi wa maeneo hayo huwakataa. Tushawahi kushuhudia hayo mara kwa mara. Tulishuhudia hayo katika Vita vya Iraq katika maneo kama vile Mkoa wa Anbar ambako makabila ya Kisuni yalibadilima mara moja na kuazi kwa sababu ya mwongozo wa itikadi kali," Rais Obama alisema.

Post a Comment

emo-but-icon

item