Wandishi wa Al Jazeera miaka 7 jela
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/wandishi-wa-al-jazeera-miaka-7-jela.html
Mahakama nchini Misri
imewahukumu jela miaka saba wandishi watatu wa habari wa shirika la
habari la Al Jazeera waliokuwa wamezuiliwa kwa miezi sita nchini humo.
Walipatikana na hatia ya kueneza habari za kupotosha na kushirikiana na kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Muslim Brotherhood.Mmoja wa wandishi hao ni Peter Greste, raia wa Australia na ambaye pia alikuwa mwandihi wa habari wa BBC wakati moja.
