Ufaransa 5-2 Switzerland
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/ufaransa-5-2-switzerland_20.html
Ufaransa imejikatia tikiti ya kusonga mbele ikiongoza kundi E licha ya kuwa na mechi moja imesalia dhidi ya Equador .
Switzerland imebakia ya pili ikiwa na alama tatu
na hivyo hainabudi kushinda mechi yao ijayo dhidi ya honduras
kujihakikishia nafasi katika 16 bora.Olivier Giroud alifunga bao la kwanza kwa kichwa katika dakika ya kumi na saba naye Blaise Matuidi akafunga la pili sekunde chache baadaye
Karim Benzema alipewa penalti lakini mkwaju wake ukazuiwa na kipa wa Uswisi, Diego Benaglio.
Yohan Cabaye aliurudisha mpira baada ya kuokolewa na Benaglio, ila uligonga juu ya lango la Uswisi.
Ufaransa waliongeza bao la tatu kabla ya muda wa mapumziko.
Valbuena hakupoteza nafasi hiyo na akautia mpira kwenye wavu wa timu ya Uswisi.
Katika dakika ya 67, Benzema alikosoa kosa lake la kutofunga penalti kwa kufunga bao lingine baada ya kupokea pasi kutoka kwa Paul Pogba.
Hilo likawa bao la nne bila jibu kwa timu ya Ufaransa.
Kisha Benzema akachangia katika kufunga la tano kwa kumpa Moussa Sissoko pasi ambayo Sissoko alitia wavuni.
Katika dakika za mwisho, timu ya Uswisi ilifanikiwa kupata mabao ya kufutia chozi hata ingawa hayakua na uwezo wa kurekebisha matokeo ya mchuano huo.Blerim Dzemaili alipiga mkwaju wa adhabu uliopita safu ya ngome ya Les Bleusna kuingia
23:52 Ufaransa 5-2 Switzerland
23:51Mechi imekamilika huku bao la Karim Benzima likikataliwa katika sekunde ya mwisho wa mechi hiyo.
23:46 Ufaransa 5-1 Switzerland 87
23:46 Xhaka anaifungia uswisi bao la pili
23:42 Blerim Dzemaili anafunga kutoka kwenye Freekick
23:51 Blerim Dzemaili anaifungia Uswisi bao la Kufutia Machozi
23:40 Ufaransa 5-1 Switzerland 81''
23:39 Uswisi wanapata bao la kufutia machozi
23:34 Ufaransa 5-0 Switzerland 73''
23:30 Moussa Sissoko anaifungia Ufaransa bao la 5
23:30 GOOOOOOAL
23:30 Ufaransa wanafanya mashambulizi tena
23:30 Patrice Evra anapoteza nafasi ya kuifungia Ufaransa bao la tano
23:28 Ufaransa 4-0 Switzerland 68'
23:24 Karim Benzema anaifungia Ufaransa bao la nne akisaidia na Paul Pogba
23:22 Mamoudo Sakho anaondoka uwanjani
23:18 Ufaransa bado wanaongoza kwa mabao matatu ya kipindi cha kwanza
23:17 Benzema anapiga nje
23:17 Evra anafungua kwa kasi shambulizi la Ufaransa
23:16 Freekick kuelekea lango la Ufransa ,Giroud ndiye mwenye kosa
23:14 Shakiri anapa mpira wa kutupwa kuelekea lango la Ufaransa
23:13 Gökhan Inleranaongoza mashambulizi ya Waswisi lakini wapi inazimwa tena na Sissoko
23:09 Switzerland wanapata kona wakiendelea kuuliza Ufaransa maswali
23:09 Ufaransa 3-0 Switzerland
23:06 Giroud anapoteza nafasi ya kukamilisha kichapo hicho
23:04 Ufaransa bado wanaongoza kwa mabao 3-0 Switzerland
23:03 Switzerland wanafanya mashambulizi ya mapema .
23:02 Kipindi cha pili kinaanza Fonte Nova
22:45+2 Ufaransa 3-0 Switzerland
22:45+2 Benzema anafanya shambulizi la mwisho kabla ya kipa kupiliza kipenga cha mwisho
22:45 Kipindi cha kwanza kimekamilika
22:44 Switzerland sasa wanaogopa kufanya mashambulizi huku wakifahamu kasi wanayoshambulia nayo hawa wafaransa
22:41 Ufaransa 3-0 Switzerland
22:40 Ufaransa wanapata bao la tatu baada ya fastbreak
22:40 GOOOOOOOAL
22:32 Benzema anapoteza penalti
22:31 Ufaransa wanapata Penalti
22:31 Bemzema anaangushwa na refarii anasema ni penalti
22:30 Benzema anashambulia lango la Switzerland
22:30 Ufaransa 2-0 Switzerland ''
22:28 Shakiri anapoteza nafasi ya wazi ya kufunga bao la kwanza la Switzerland
22:27 Bao la Switzerland lililofungwa na Xhaka linakataliwa
22:26 Offside !
22:26 Freekick kuelekea lango la Switzerland
22:24 Ufaransa inaendelea kutekeleza mashambulizi kwa safu ya Switzerland
22:19 Ufaransa 2-0 Switzerland
22:18 Balise Matuidi anaifungia ufaransa bao la pili
22:17 Ufaransa 1-0 Switzerland
22:16 Olivier Giroud (France)
22:16 GOOOOOAL
22:15 KONA kuelekea upande wa Switzerland
22:04 Switzerland inalazimika kufanya badiliko la mapema baada ya Steve Von Bergen Kujeruhiwa na Cohan Cabaye
22:03 Kocha wa Switzerland Ottmar Hitzfeld anatafuta tikiti yake ya kwanza ya 16 bora
22:03 Mechi imeanza
22:00 Ufaransa ilishinda mechi yake ya kwanza 3-0 dhidi ya Honduras
22:00Ufaransa inapambana na Switzerland katika mechi ambayo lazima washinde ilikuimarisha nafasi ya kusonga mbele katika raundi ya pili ya kombe la dunia