UBELGIJI YAICHAPA URUSI 1-0 NA KUFUZU HATUA YA 16 KOMBE LA DUNIA
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/ubelgiji-yaichapa-urusi-1-0-na-kufuzu.html
Bora kuchelewa kuliko kutofika: Divock Origi akifunga bao lake la ushidni zikiwa zimesalia dakika 2 mpira kumalizika.
Imechapishwa Juni 22, 2014, saa 3:00 usiku
MCHEZAJI
kinda aliyetokea benchi, Divock Origi ameifungia bao pekee Ubelgiji
ikishinda 1-0 dhidi ya Urusi usiku huu katika mchezo wa kombe la dunia.
Haikuwa
rahisi kwa Ubelgiji kupata matokeo, lakini zikiwa zimesalia dakika
mbili mpira kumalizika, kinda huyo mwenye miaka 19 alifunga bao muhimu
akimalizia kazi nzuri ya Eden Hazard.
Ushindi huo umewafanya Ubelgiji kuongoza kundi H kwa kujikusanyia pointi 6 na kwa maana hiyo wameshafuzu hatua ya 16.
Origi akipongezwa na mchezaji mwenzake Kevin Mirallas
Kikosi cha Urusi: Akinfeev, Kozlov, Ignashevich, Kanunnikov, Glushakov, Kokorin, Berezutskiy, Shatov, Samedov, Fayzulin, Kombarov