TCRA YATOA ONYO KWA WANAOTUMIA MITANDAO KUCHAFUA WENGINE
Dr. Raynold Mtungahema
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/tcra-yatoa-onyo-kwa-wanaotumia-mitandao.html
Dr. Raynold Mtungahema |
Mamlaka
ya mawasiliano nchini, TCRA, imewaonya wale wote wanaotumia mitando
kuchafua na kudhalilisha watu waache mara moja vinginevyo watakabiliwa
na mkono wa sheria.Onyo hilo
limetolewa jana mjini Arusha na Kaimu Mkurugenzi wa mamlaka ya
mawasiliano nchini TCRA, Dkt, Raynold Mtungahema, alipokuwa akitoa
ufafanuzi wa maswali ya wanahabari kuhusu kuenea kwa picha chafu
zinazowadharirisha watu mbalimbali kwenye mitandao.Nilipata
kufafanua yakua mtandao au kifaa chochote cha digitali kinapotumiwa
visivyo kinaweza kupelekea mtumiaji kujikuta akifanya uhalifu mtandao.
Mifano katika hili nilipata kueleza, pale mtumiaji anapotumia mtandao
kutukana, kutishia na kudhalilisha wengine mitandaoni anakua amefanya
kinachoitwa "Cyberbullying" ambacho ufafanuzi wa hili unaweza kusomeka
Kwa
nchi za magharibi wamekuwa na kampeni mbali mbali zinazo hamasisha
kutokomeza aina hii ya uhalifu mtandao ambapo takwimu za ITU za mwaka
2013 zilionyesha takriban nusu ya wenye umri kati ya miaka 13 - 17
wamekua wana athirikazaidi na "Cyberbullying".
Kwa
Tanzania hapakua na tofauti, Mitandao imekua ikitumika kusambaza
taarifa za uongo, chuki na kudhalilisha wengine na hata baadhi kutishia
wengine kupitia mitandao (Simu pamoja na Komputa) kitu ambacho ni hatari
sana kwa usalama wa taifa lolote. Hili lilipelekea TCRA kuja na kampeni
ya "Futa delete kabisa" inayo hamasisha kutosambaza jumbe za chuki,
matusi au uongo ili kulinda amani ya Tanzania.
Aidha,
hapo jana Katika muendelezo kuhakiki yakua kunakua na matumizi salama
ya mitandao Dr. Mtungahema amesema, matumizi ya mitandao ambayo sio
sahihi ni kosa la jinai na hivyo wale wote wenye tabia hiyo waache mara
moja na akawataka wanaochafuliwa
kupitia mitandao wafungue majalada polisi na mamlaka hiyo itasaidia
kuwafuatilia wahusika na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria .
Alisema
mitandao yote imesajiliwa hata kama aliyehusika kuchafua anaishi
uvunguni atakamatwa kwa kuwa mitandao haipo kwa ajili ya matumizi yasiyo
sahihi ambayo hayaruhusiwi.
Mtungahema,
amesema atakaebainika anatumia mtandao kumchafua mtu mwingine huyo
amefanya kosa la jinai hivyo afikishwe mbele ya vyombo vya sheria kwa
kuwa tayari zipo sheria zinazotoa adhabu kwa mtuhumiwa atakaepatikana na
hatia.
Aliongeza
kuwa TCRA, imeshapokea malalamiko mengi na tayari wahusika wameshatiwa
mbaroni na ufuatiliaji utaendelea ili mradi tu mamlaka hiyo itaarifiwe.
Nchi
wanachama wa jumuia afrika mashariki zimeaanza kikao cha siku nne
mjini Arusaha kwa ajili ya kutafuta ufumbuzi wa chang moto mbalimbali
zinazoikabili sekta ya mawasiliano.
Mwenyekiti
wa jumuia hiyo ya sekta za mawasiliano, EACO, Dakta Fracis Wangusi,
amesema sekta ya mawasiliano inakabilwa na changamoto mbalimbali ambazo
zinakwamisha upatikanaji wa huduma za mawasiliano kwa haraka.
Wangusi
ambae pia ni mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya mawasiliano nchini
Kenya,amezitaja sekta hizo kuwa ni pamoja na kuhama kutoka mtandao wa
analojia kwenda digital na matumizi ya visumbusi kwa ajili ya luninga.
Aliongeza
kuwa , sekta ya simu inakabiliwa na changamoto ya kuwepo gharama kubwa
za matumizi ya simu, usambazaji barua na vifurushi kunakofanywa
namashirika ya posta unaotokana na ukuaji wa mji ambao haujapangiliwa
,matumizi ya vikwazo vya kuchelewesha huduma ya haraka ya internet .
Alisisitiza kuwa ili kupatikana kwa mafanikio hayo ni kuondoa vikwazo na kuhimiza uwekezaji kwenye sekta ya mawasiliano ICT.